Siuoni uchaguzi bali natarajia uchafuzi

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein

HATA nami naamini hakutakuwa na uchaguzi wenye tija Zanzibar itakapofika 20 Machi.
Sababu zipo wazi kwa kuwa mpaka sasa si Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) wala Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), iliyotoa ushahidi popote pale kuwa uchaguzi mkuu wa 25 Oktoba 2015, uliharibika.

Kama hakuna ushahidi huo, na imethibitishwa mara nyingi kuwa hata Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachoshikilia kwa kila hali uchaguzi huo wa marudio, ikiwemo viongozi wake kutumia lugha ya kulaghai na kukejeli, kimeshindwa kuwasilisha ushahidi huo.

Ipo haki ya kutajwa kwa chama hiki kwa sababu ndicho kilichoshutumu Tume ya Uchaguzi kwa ilichodai kuvuruga taratibu za uchaguzi, na kwa sababu hasa kwamba ndicho kinachojulikana kusaka huruma isiyostahili ili kutangazwa mshindi bila ya kuchaguliwa na wananchi.

Kwa sababu hiyo basi, ina maana hakuna uhalali wa uchaguzi huo ulioitishwa na Jecha Salim Jecha, ambaye kwa maadili ya utumishi wa umma, na kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar (1984), na Sheria ya Uchaguzi Zanzibar Na.11 (1984), ni mtuhumiwa wa kuhujumu uchaguzi halali na kusababisha fadhaa kubwa ya kiusalama.

Hakuna uhalali wa uchaguzi wa marudio alioutangaza kwa staili ileile ya kukaa mafichoni akatangaza kufuta uchaguzi ule, kwa sababu pia mpaka leo, hakuna ushahidi wa vielelezo vya kisheria kuonesha alikuwa na mamlaka ya kufanya alichofanya 28 Oktoba 2015.

Kwa tuhuma hizo zinazomgusa Jecha, kada wa CCM aliyegombea nafasi ya kuwania ubunge jimbo la Amani, mjini Zanzibar katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, pangekuwa na uongozi uliotimia akili na uungwana, angekuwa mikononi mwa vyombo vya dola anahojiwa ili kushitakiwa.

Ni kwa sababu tu Zanzibar, chini ya uongozi wa zaidi ya miaka 50 wa CCM, imekuwa ikiongozwa kwa misingi ya siasa za fitna na chuki dhidi ya wale wanaotajwa hawakushiriki mapinduzi ya 12 Januari 1964, na kwa hivyo wakichukuliwa kuwa wanawakilisha mawazo ya waliopinduliwa kama nilivyonukuu maneno yaliyoandikwa na kusemwa yametoka kinywani mwa Balozi Amina Salum Ali.

Huyu Balozi Amina anasema katika mgogoro uliopo Zanzibar, tatizo ni Maalim Seif Shariff Hamad anayedai “haelewi dhana ya maelewano, yuko serikalini siyo kwa ajili ya maendeleo bali kupeleleza serikali ya CCM inafanya nini ili aikosoe. Sasa huo ni unafiki.”

Anasema “Tatizo sio CUF, ni Maalim Seif ambaye mazingira yanaonesha ana maslahi binafsi na siyo ya Wazanzibari.” Haya yamo kwenye gazeti la Mwananchi, 30 Januari, 2016, kutokana na mahojiano yaliyofanywa Balozi Amina akiwa amefuatana na Abdalla Rashid Abdalla (Mkuu wa Mkoa mstaafu), Mohamed Hijja (Balozi mdogo wa Tanzania nchini India aliyewahi kuwa naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa) na Fatma
Maghimbi.

Maelezo hayo ambayo kwa mwanamama huyu mtaalamu wa uchumi, ni zaidi ya kujipigia kampeni ya kupata uwaziri, ni sehemu ya propaganda chafu dhidi ya Maalim Seif ambaye takwimu zilizo mikononi mwa ZEC, zinamuonesha ameshinda uchaguzi, isipokuwa anadhulumiwa na viongozi wa CCM kwa kuogopwa kuwa ataibadilisha Zanzibar kutokana na dhamira njema aliyonayo.

Lakini isitoshe, maelezo ya Balozi Amina yanathibitisha maandalizi ya CCM na washirika wake vyombo vya ulinzi na usalama, kutumia mgongo wa uchaguzi wa marudio kumtangaza mgombea wao, Dk. Ali Mohamed Shein, ili aongoze serikali itakayoruhusu kuvunjwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa (SUK) ulioridhiwa na umma kwa asilimia 66.4 ya kura huku ukiwachukiza wanasiasa wahafidhina wa chama hicho.

Mazingira hayo ndiyo yanadhihirika leo baada ya Jecha kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio. Askari wamerudi kurandaranda mitaani, wahuni waliovalia soksi usoni ambao wanaaminika wanaingia mitaani kwa maelekezo ya uongozi wa juu wa CCM, na kazi yao ni pamoja na kutisha wananchi ambao wanasiasa wachovu wanawahimiza wajitokeze kushiriki uchaguzi huo.

Staili ya kishetani kusema kweli – eti viongozi wa chama kinachodhulumu haki ya wananchi kuchagua viongozi wanaowataka, kiagize askari wa serikali watishe na kudhalilisha wananchi, ili wananchi hao waje kushiriki uchaguzi kwa amani. Hii ndio hasa ndoto ya alinacha.

Wananchi wabaguliwe kwa kuitwa machotara wasiohitajika Zanzibar, nawanaotajwa kuwa warudi kwao Pemba, kwa kutumia meli mpya ambayo imeonekana labda ni kuukuu, lakini ikidaiwa kununuliwa kwa bei isiyostahili, ya Dola 30 milioni, mpaka kuwashangaza wahandisi wa majini wa kimataifa.

Uwanyime haki ya kuandikishwa ili kuingia kwenye daftari la kudumu la wapigakura, kwa visingizio hivi na vile, vilivyojengwa katika mfumo wa sheria dhalili, halafu uwatake wapuuze msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa (BKUT) la CUF la kutoshiriki uchaguzi wa marudio.

Ni mjinga tu atakayeamini kuwa kwa kuitisha uchaguzi huo, viongozi wa serikali ambao wengi wao ndio waandamizi katika uongozi wa CCM, wana nia njema ya kuwapatia wananchi wa Zanzibar viongozi bora kwa mujibu wa Katiba.

Ni katiba ipi wanaitii viongozi ambao wanamshikilia Jecha kama mfungwa huku wakimuagiza kuchomoza kichwa na kutoa matangazo ya kuongeza utata katika mgogoro walioutegeneza kwa ushirikiano?

Katiba ya Zanzibar inataka uamuzi wa Tume uwe ni ule uliopitishwa na kikao kilichoitishwa na kusimamiwa na ama Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti, na makamishna wasiopungua wanne. Mbona ushahidi wa kikao hicho kabla ya kufikiwa uamuzi haupo?

Na je mbona wakati Jecha alipotelekeza wenzake katika Tume siku ya 28 Oktoba na kuja kuibuka kupitia Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC), akisema ameufuta uchaguzi uliofanyika siku tatu kabla, hakusema alifanya vile kwa sheria ipi?

Na kama viongozi wa CCM ni waadilifu na wakweli wa nafsi zao, ni kwa nini basi mpaka sasa wanaendelea kumshikilia Jecha mafichoni kama vile mtoto mwenye maradhi ya wasiwasi? Yeye si ni mwenyekiti wa tume, arudi tu kazini ili hiyo mipango ya uchaguzi wa marudio aifanyie ofisini na sio akielekezwa na wanaomhifadhi?

Leo Zanzibar inafikishwa kuingia katika uchaguzi unaoandaliwa ndani ya mazingira ya hofu na vitisho kwa kiongozi wa asasi ya kisheria ya kusimamia uchaguzi, huku Sekretarieti ya Tume ikiwa chini ya ulinzi au maelekezo ya wakubwa wa CCM, chama kile kinachotaka kulazimisha njia yake.

Ni hali ya hatari isiyokubalika katika nchi iliyoweka katiba inayoelekeza Zanzibar kuwa ni nchi inayofuata misingi ya kidemokrasia ikiwemo kupata viongozi wake wa serikali kupatikana kwa njia ya uchaguzi, njia ambayo inalelewa na Sheria ya Uchaguzi.

Sheria ya Uchaguzi imeshafinyangwa ulimwengu ukishuhudia, na ni kwa utashi wa CCM, walawale wanaohangaika kujibakiza madarakani. Hakutakuwa na uchaguzi bali uchafuzi.

Chanzo: MwanaHalisi

One Reply to “Siuoni uchaguzi bali natarajia uchafuzi”

  1. Wanataka matakwa ya mtume wao yatimie ya kuiteka na kuimiliki Zanzibar kupitia Waafrika wenzao wa Afrika associatioin walioselelea Zanzibar na kujifanya wazanzibari. Kila anaejiita ni Mwafrica hapa Zanzibar hana asili napo ni wakuja na hao ndio wanaowadhallilisha wazanzibari asilia wa nchi hii.
    Washenzi hawa wakifanya machafuzi yao na kujitangaza basi atakae wapinga atitwa haini na watamdhalilisha kwa kufungwa bila huruma kwani hawa damu zao ni za kishenzi hawaoni haya wala vibaya.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s