Haki yenu haitapotea Inshaallah- Maalim Seif

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na wageni wake Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, Prof Ibrahim Lipumba na Mzee Moyo katika hafla ya Maulid ya Mtume (s.a.w)
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na wageni wake Rais Mstaafu wa Zanzibar, Amani Karume, Prof Ibrahim Lipumba na Mzee Hassan Nassor Moyo katika hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (s.a.w) iliyofanyika Bwawani Zanzibar

Salma Said

 

Zanzibar: Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad amesema mazungumzo ya vikao vinavyoendelea yataleta ufumbuzi utakaozingatia katiba na sheria za nchi na kuwataka wananchi kuomba dua huku wakiamini haki yao haitapokea.

 

Aidha amewataka wazanzibari kutulia na kusubiri maamuzi ya vikao hivyo vinavyofanyika Ikulu Mjini Unguja ambapo alisema ana imani kubwa na mazungumzo hayo juu ya kuleta ufumbuzi wa mgogoro unaofukuta tokea kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi Octoba 28 mwaka jana na Mwneyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jecha Salum Jecha.

 

Kauli hiyo ameitoa Maalim Seif wakati akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu waliohudhuria katika maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (s.aw) yaliofanyika katika ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani.

 

“Mazungumzo yanayoendelea nategemea yataleta ufumbuzi wa haki utakaozingatia matakwa ya katiba na sheria, lakini pia maamuzi ya wananchi walioyatoa kupitia kisanduku cha kura yataheshimiwa Inshaallah” alisema Maalim Seif huku wananachi wakiitikia Inshaallah.

 

Maalim Seif alisema tokea kumalizika kwa uchaguzi Octoba 25, 2015 kuna vituko vingi na vitimbi vya kila namna lakini jambo la kushukuru wananchi wametakiwa kutulia na wametulia bila ya kuonesha hasira za aina zozote.

 

Hata hivyo amewataka wananchi kutokubali kuchokozwa na wakachokozeka kutokana na uchokozi unaofanywa kwa makudusi ukiwa na lengo la kuamsha hasira ambazo zitapelekea kuvunjika kwa hali ya amani nchini.

 

“Najua mambo mengi yamefanyika na lengo lake mnachokozwa ili mchokozeke na hali ya amani ivunjike lakini nakuombeni msichokozeke na kama mlivyovumilia endeleeni tena uvumilivu na msivunjike moyo na inshallah kheri itapatikana” aliongeza Maalim Seif huku wananchi wakimsikiliza na kuitikia amini kwa kunyanyua mikono juu.

 

Maalim alisema wakati huu wa mazungumzo wapo waliozungumza mambo mengi na wataendelea kuongea hadharani mambo mbali lakini lakini aliwataka wananchi kutoyazingatia kwa kuwa yanataweza kusaidia kuleta hali ya amani zaidi ya kuleta taharuki na kuzidisha hasira kwa wananchi.

 

Alisema majaribio mengi yameshafanyika ili hali ya amani itoweke lakini jambo zuri wananchi wamekuwa watulivu na wanataka amani iendelee kuwepo licha ya mambo yote bado wametulia na kuwapongeza kwa hatua hiyo ambayo amesema ina mazingatia makubwa kwa viongozi ambao wanachochea wananchi ili kuamsha hasira.

 

Maalim Seif alikuwa akiongea hayo wakati alipowakaribisha katika chakula cha mchana baada ya kumalizika kwa maulidi ya Mtume Muhammad (s.w.a) ambapo hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Professa Ibrahim Lipumba, Rais Mstaafu Dk Amani Abeid Karume na Mzee Hassan Nassor Moyo.

Baadhi ya viongozi wengine wa serikali walioalikwa hawajahudhuria kama ilivyokuwa kawaida katika shughuli hiyo ambayo hufanyika kila mwaka ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya mazazi ya Kiongozi wa Waislamu Mtume Muhammad (s.a.w).

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Advertisements

One Reply to “Haki yenu haitapotea Inshaallah- Maalim Seif”

  1. Bado waZanzibar wanaanchwa njia panda na viongozi wao ..kwani bila ya kuwepo na deadline policy ya vikao hivyo na bila ya kuwepo Na maelezo ya mukhtasari ya mazungumzo hayo yanayowashirikisha viongozi wa juu wa serikali ….hiyo itakuwa ni sawa na filamu ya sinema inayoonesha pasi na kuwepo sauti !!! Kwani mwananchi ana HAKI nae kujulishwa japo in brief hatua zilizochukuliwa na yepi yaliokubalika

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s