Kusanyeni zaka na sadaka zinufaishe jamii

Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya kukusanya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Shekh. Said Masoud (Gwiji) akitoa maelezo ya Jumuiya na kumkaribisha mgeni rasmi (kushoto) Katibu Mtendaji Kamisheni ya Wakfu na Mali ya amana Zanzibar Shekh. Abdalla Talib kufungua Mkutano wa Jumuiya hiyo uliofanyika katika ukumbi Sha-Ntimba Mombasa Zanzibar.Picha na Makame Mshenga

Taasisi za Kiislamu nchini zimeshauriwa kushawishi kuwepo kwa mfumo wa pamoja wa ukusanyaji wa Zaka na Sadaka ili ziweze kuleta tija katika kundi kubwa la jamii ya Kiislam halina uwezo kimaisha.

Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar, Sheikh Abdalla Talib amesema lengo la mfumo huo uliwekwa kwa mujibu wa sheria za kiislamu ni kukusanya fedha hizo kutoka kwa watu mbali mbali ili kusadia na kupunguza umasikini katika jamii ambayo inakabiliwa na maisha magumu.

 

Hata hivyo alisema lengo hilo halijafikiwa kutokana na kuwa baadhi ya watu wengi wanaotoa sadaka hizo hazifikii lile lengo lililokusudiwa kwa vile kumekosekana mfumo bora  unaowafikia watu wengi na kuleta mabadiliko makubwa katika jamii hiyo ya kiislamu.

Akifungua mkutano wa Jumuiya hiyo ya Zaka na Sadaka Zanzibar (JUZASA) Sheikh Talib ametolea mfano wan chi tofauti kama Denmark ambako licha ya kuwepo asilimia ndogo ya Waislamu kama 3% lakini imeweka utaratibu mzuri wa ukusanyaji wa Sadaka na Zaka jambo ambalo husaidia kwa kiasi kikubwa fedha hizo kupelekwa kwa wale watu wenye mahitaji ndani ya nchi hiyo na hata nje ya nchi hiyo.

 

Zanzibar ambayo ina wasilamu asilimia 99% ilipaswa kuwa ni mfano wa nchi nyengine lakini amesema bado elimu ya kutekeleza ibada hiyo muhimu haijawafikia watu wengi nab ado wenye uwezo hawajaamua kufuata utaratibu huo ambao umewekwa katika mafundisho ya Bwana Mtume Muhammada (s.a.w) wa kuwasaidia watu wasio na uwezo katika jamii.

 

Mwenyekii wa Jumuiya hiyo, Sheikh Said Masoud (Gwiji) bado muamko wa watu wenye uwezo kutoa Sadaka na Zaka lakini elimu ya umuhimu wa jambo hilo unahitajika ili watu wenye uwezo wahamasishwe waweze kujitolea kutoa sadaka zao kwa ajili ya kuwasaidia wale wasio na uwezo.

 

“Bado muamko ni mdogo sana hasa kwa ndugu zetu Wafanyabiashara kutoa zaka na sadaka wanaona tabu sana lakini hili jambo ni ibada na linatakiwa litiliwe nguvu kwani fedha na vitu vinavyotolewa zaka vinapelekwa kwa wale wenye mahitaji ambao hawana uwezo kwa hivyo natoa wito kwa wenye uwezo kutekeleza ibada hii muhimu” alisema Sheikh Masoud.

 

Kwa upande wake Katibu wa Jumuiya hiyo ya JUZASA, Sheikh Omar Abubakar Mohamed amesema jumuiya hiyo imeshatoa zaka kwa watu 46 zikiwemo za fedha taslim, na vitu vyengine kama Vyarahani, Friza na baadhi ya watu tayari wameshajengewa nyumba za kuishi na familia zao.

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s