Hasara ya zaidi Billioni 200 mashamba ya Miwa

Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  Bwana Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara iliyopatikana kutokana na hujuma ya moto kwenye mashamba ya Miwa Mahonda.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda BW. Tushar Mehta akimueleza Balozi Seif hasara iliyopatikana kutokana na hujuma ya moto kwenye mashamba ya Miwa Mahonda.

Wafanyakazi 350 wapo hatarini kukosa ajira kufuatia baadhi ya watu kuamua kwa makusudia kuchoma moto mashamba ya Miwa yaliopo kwenye Kiwanda cha Sukari kilichopo Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Meneja wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda,  Tushar Mehta alisema hayo wakati akimueleza, Balozi Seif Ali Iddi aliyefika kuangalia hasara iliyosababishwa na moto uliotiwa kwa mara nyengine tena na Watu wasiojuilikana  ndani ya shamba la Miwa katika kipindi cha siku tano baada ya tukio kama hilo la Disemba  30 mwezi uliopita.

Baadhi ya Miwa iliyoteketea kwa moto kutokana na hujuma iliyofanywa  na Watu wasiojuilikana huko kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Baadhi ya Miwa iliyoteketea kwa moto kutokana na hujuma iliyofanywa na Watu wasiojuilikana huko kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kitendo hicho cha hujuma kinaweza kuusababisha Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  kuwa na mawazo ya kufikiria kuzuia ajira mpya 450 za Wafanyakazi wa Kiwanda hicho katika malengo yake baada ya kukamilika kwa matengenezo makubwa na kuanza tena uzalishaji wa sukari.

 

Tushar alisema moto huo umetiwa kati kati ya shamba la Miwa  jana jioni na wahalifu wenye  dhamira ya makusudi ya kutoa usumbufu na kizuizi kwa wananchi na vikosi vya Ulinzi katika harakati za kukabiliana na moto huo.
Alisema Eka zipatazo 50 za Miwa iliyopevuka imeteketea kwa moto hali ambayo imeisababishia Kiwanda hicho hasara ya Tani 200 za Sukari na Lita 2,300 za Spititi zilizokuwa zizalishwe kutokana na miwa hiyo ikiwa na hasara  ya jumla ya dola za Kimarekani Laki 228,758.56 sawa na zaidi ya shilingi Milioni 494 za Kitanzania.

Meneja huyo wa Mradi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda  alifahamisha kwamba hadi sasa Eka zipatazo 200 zimeteketea  kwa moto kwenye  matukio yote mawili  katika kipindi cha siku Tano zilizopita na kusababisha hasara ya jumla ya Dola za Kimarekani  Milioni 1,176,234.28  sawa na shilingi za Kitanzania  Bilioni 2,326,818,500/-.

Akiupa pole Uongozi wa Kiwanda cha Sukari Mahonda kutokana na hasara  ya Mashamba  iliyosababishwa na moto  huo Balozi Seif alisema hujuma hiyo ya makusudi haiitakii neema Zanzibar katika harakati zake za kustawisha uchumi wake.

Balozi Seif aliwanasihi watu wenye tabia hiyo kuachana nayo kwani mbali ya kujibebesha dhambi lakini pia inawavunja moyo wawekezaji walioamua kuja kuwekeza miradi yao ya kiuchumi  Nchini kwa lengo la kuisaidia Serikali pamoja na Wananachi hapa Zanzibar.

Alisema kwamba juhudi za makusudi za Serikali kuu katika kukifufua tena Kiwanda cha Sukari  na Manukato Mahonda baada ya kusita kwa miaka kadhaa zililenga kuimarisha  Uchumi kupitia sekta ya viwanda sambamba na kupanua  soko la ajira kwa Vijana.

Alisema tabia ya baadhi ya watu kufikiria kwamba hujuma hiyo itatoa fursa kwao kutumia maeneo ya mashamba ya Miwa kuendeleza Kilimo na Mifugo inafaa kuachwa mara moja kwa vile mashamba hayo yataendelea kuwa katika mipango ya  Serikali ya kuhudumia  Sekta ya Viwanda.

“Haya ni Mashamba ya Serikali yaliyotengwa maalum kwa shughuli za harakati za Viwanda. Hivyo ndoto za baadhi ya Watu kufikiria kwamba  hujuma zao zitazaa matunda kwa kufanya wanavyotaka zinapaswa ziachwe mara moja ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif aliuambia Uongozi wa Kiwanda hicho kwamba Serikali inaangalia mpango utakaowezesha Vikosi vya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kusaidia ulinzi kwenye Mashamba hayo ili kulinda hujuma zinazoonekana kushamiri siku hadi siku.

Hilo ni tukio la sita la hujuma za moto kwenye mashamba ya Miwa ya Kiwanda cha Sukari Mahonda  tokea kianze tena uzalishaji wa sukari na Spiriti mapema mwaka uliopita wa 2015 ambapo kumekuwepo na matatizo kati ya wawekezaji na wenyeji wa kijiji kilicho karibu na kiwanda hicho.
 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s