Siri kukwama tarehe ya uchaguzi yafichuka

Wapiga kura wakihakiki majina yao kabla ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, 2015; ambao ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha
Wapiga kura wakihakiki majina yao kabla ya kupiga kura kwenye uchaguzi wa Oktoba 25, 2015; ambao ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salim Jecha

Wakati wananchi wa Zanzibar wakiwa njiapanda baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu visiwani humo, imebainika kilichopelekea Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kukwama kupanga tarehe ya uchaguz wa marudio katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.

Taarifa za uchauzgu zilizopatikana jana mjini Zanzibar na kuthibitishwa na baadhi ya makamishina wa tume hiyo, zimedai kuwa tarehe ya kufanyika uchaguzi huo ilikwama kupangwa baada ya tume kugawanyika makundi mawili, wanaokubali kurudiwa na wanaopinga kufanyika uchaguzi huo.

Inadaiwa katika kikao hicho cha siku mbili kilichofanyika makao makuu ya ZEC Maisara, mjini Zanzibar, tume hiyo ilishindwa kufikia muafaka wa pamoja wa kupanga tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi wa marudio baada ya kuibuka mvutano.

Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Kamishina mmoja wa tume hiyo ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake, alidai ajenda ya uchaguzi mkuu haikupelekwa rasmi katika kikao hicho, isipokuwa ilipenyezwa na waziri mmoja wa zamani.

Alisema baada ya kamishna huyo kutoa hoja ya kurudiwa uchaguzi, baadhi ya makamishina walipinga, wakitaka kufahamu sababu za kurejewa uchaguzi huo kama zimezingatia matakwa ya Katiba na sheria au unarudiwa kwa sababu za kisiasa.

Aidha, alisema wajumbe hao walifika mbali zaidi na kutaka tamko la Mwenyekiti wa ZEC la kufuta matokeo ya uchaguzi liwasilishwe katika kikao cha tume ili lijadiliwe ikiwamo kuangali kama lina  nguvu za kikatiba na sheria.

“Kutokana na hali hiyo, ZEC imelazimika kuitaka kamati tendaji  yake (Sekretarieti) kuandaa mpango kazi wa kurudiwa kwa uchaguzi na kuonyesha utaratibu mzima utakaotumika katika uchaguzi huo,” alisema.

Aliongeza kuwa, taarifa ya kamati tendaji itawasilishwa kwa tume na kujadiliwa na kikao hicho ndiyo kitakachopanga tarehe ya kufanyika uchaguzi huo baada ya kupatikana muafaka.

Chanzo: Nipashe

3 Replies to “Siri kukwama tarehe ya uchaguzi yafichuka”

  1. Wacheni kupoteza pesa na kudanganya watu. Uchaguzi ukirejewa itakua nini? Asha Bakari kakuambieni mapema serikali ya CCM haitolewi kwa karatasi. CCM imefanya mapinduzi na nyinyi fanyeni yenu muipate serikali. Hamuwezi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s