Balozi Seif: Uchaguzi wa marudio upo

Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa.
Balozi Seif ambae pia ni Mwenyekiti wa halmashauri ya maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar, akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari wakati akijibu baadhi ya maswali aliyoulizwa.

Makamo wa Pili wa rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, amesema kuwa mchakato wa kutafuta bajeti kwa ajili ya Uchaguzi wa Marejeo tayari umekamilika.

Alisema kuwa kilichobaki hivi sasa ni kusubiri kwa Tume ya Uchaguzi (ZEC) kutangaza siku ya Uchaguzi, huku akisema kuwa Chama Chake kipo tayari kushiriki Uchaguzi huo waka wowote.

Balozi Seif aliyasema hayo jana ofisini kwake wakati akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa raarifa juu ya maaadhimisho ya Sherehe za mika 52 ya Mapinduzi Zanzibar.

Alifahamisha kuwa kwa kuwa matokeo ya uchaguzi yalifutwa basi ni wazi kuwa hakuna utaratibu ambao utakaofanyika wa kuyamaliza matokeo yaliobaki na badala yake ni kusubiri kwa Uchaguzi wa marejeo.

“Ndugu zangu wananchi tuachane kusikiliza maneno ya porojo nje ‘drip’bali nawatanabahisha kuwa suala la marejeo ya Uchaguzi lipo kama kawaida na kilichobaki sasa ni kusuri amri ya tum e kwa kutangaza siku ya Uchaguzi huo”alisema Balozi.

Aliongeza kusema kuwa “kwa upande wa Chama Cha (CCM) tupo tayari kushiriki Uchaguzi huo hataka kama Chama Cha (CUF) hawatoshiriki sisi hawatubbaishi”.

Kwa upande wa mazungumzo yanayofanyika Ikulu kwa kuwashirikisha viongozi wa wakuu wa Serikali na Maalim Seif Sharif Hamad alisema kuwa yeye hajui nini kinaendelea hadi sasa ila wananchi wasubiri mazungumzo hayo yatakapomalizika taarifa rasm itatolewa.

“kikubwa zaidi nlichokisikia mimi katika mazungumzo hayo panazungumzwa suala la kudumiha amani na utulivu ila kwa upana zaidi tusubiri mazungumzo hayo yatakapomalizika taarifa itatolewa kwa wananchi wote”alisema Balozi.

Hata hivyo Balozi Seif kwa upande wa sherehe za miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar alisema kuwa  pamoja na viongozi wa Chama Cha (CUF) kutangaza kutoshiriki katika Maadhimisho ya miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoshiriki kwao hakutoathiri kitu chochote katika ufanikishaji wa sherehe hizo.

Alisema kuwa pamoja na kauli yao hiyo kamati ya maadalizi ya sherehe ya sherehe na mapambo tayari imeshajipanga vya kutosha na kilichobaki hivi sasa ni ufanikishaji ya maadhimisho hayo ambapo shamrashamra zake zinatarajiwa kuanza rasm leo.

Alisema kuwa kuwa madhimisho hayo yapo kama kawaida na mwaka siku ya kwanza ya shamrashamra zake wamepanga kuitumia siku hiyo yaani ni leo kwa kufanya suala la usafi wa mazingira katika maeneo mbali mbali ya mji wa Zanzibar.

Alisema kuwa usafi huo utakuwa ni sehemu ya shamrashamra hizo ambapo sehemu zinazotoa huduma za kijamii kama vile Hospital,Makoni,Madukani nakhalika zitakuwa ni kipaumbele kwa kuzifanyia usafi huo.

Alifahamisha kuwa shamrashamra nyengine za maadhimisho hayo zitaendeleo kama kawaida kwa kufungua miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kuweka mawe ya msingi Unguja na Pemba.

Sherehe hizo za kutimiza miaka 52 ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu zimebeba ujumbe usemao kuwa ‘Mapinduzi Daima’ ambapo kilele chake kinatarajiwa kufikia january 12 katika viwanja vya Amani Mjini Unguja

Chanzo: OMPR

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s