Wazanzibari wametulia, wanasiasa wasiwachanganye

Vijana wa Zanzibar wakionsha furaha baada ya kutangazwa majimbo ya Tume ya Uchaguzi wa Octoba 25 mwaka huu
Vijana wa Zanzibar wakionsha furaha baada ya kutangazwa majimbo ya Tume ya Uchaguzi wa Octoba 25 mwaka huu

Kwa ufupi

Taarifa zilisema kikao hicho kiliongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Kamati maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM, upande wa Zanzibar juzi ilikutana kwa msaa nane (kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni), na kutoa tamko la kuwataka wafuasi wake visiwani kujiandaa na uchaguzi wa marudio wa Rais wa Zanzibar na wawakilishi.

Taarifa zilisema kikao hicho kiliongozwa na makamu mwenyekiti wa CCM na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wa Serikali.

Lakini kubwa zaidi ni taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na katibu wa itikadi na uenezi wa kamati maalumu ya NEC, Waride Bakari Jabu akisema kikao hicho kimewataka wana-CCM kunza kujiimarisha, kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza kwa wingi kwenye uchaguzi wa marudio ili kuipa CCM ushindi Zanzibar, kuanzia urais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani.

Wakati CCM ikitoa tamko hilo, tayari kuna mfululizo wa vikao vimefanyika Ikulu ya Magogoni ambako Novemba 4, Rais wa zamani wa Jamhuri ya Muungano, Jakaya Kikwete alikutana na katibu mkuu wa CUF, Seif Shariff Hamad kuzumgumzia hali ya kisiasa Zanzibar.

Taarifa ya Ikulu ilisema mazungumzo hayo yalitokana na maombi ya muda mrefu ya Maalim Seif, ambaye pia ni makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar (SUK). Pande hizo zilikubaliana kuwa mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yaendelee.

Desemba 21, Rais John Magufuli alifanya mazungumzo Ikulu na Maalim Seif kuhusu hali ya kisiasa visiwani, na wote walifurahia hali ya usalama na utulivu inayoendelea.

Taarifa ya Ikulu ilisema Rais Magufuli aliwapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu, wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM na alimsihi Maalim Seif na viongozi wa CCM waendelee na mazungumzo hadi mwafaka upatikane.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu, Rais Magufuli na Maalim Seif kwa pamoja waliwaomba Wazanzibari waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano.

Lakini kinachoshangaza hapa, wakati kiongozi mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano akisisitiza amani na utulivu na kutoa nafasi kwa mzungumzo ya mwafaka, na upande mwingine nao ukizungumza lugha hiyo hiyo, CCM imekuja na tamko la kutaka kuichokonoa kauli ya amani na utulivu inayosisitizwa.

Kauli kwamba wana-CCM wajitokeze kwa wingi kwenye uchaguzi wa marudio inaweza kumaanisha kuwa pande zinazoendelea na mazungumzo zimeshakubaliana kuwa uchaguzi urudiwe, kitu ambacho CUF bado wanasisitiza kuwa hakijakubalika.

Kauli za namna hii hazirutubishi mazungumzo ya kutafuta muafaka, bali zinadhoofisha na kuzidi kuwaweka Wazanzibari na dunia kwa ujumla katika hali ya kutoeleweka.

Hii ni kauli ya pili kutolewa na CCM kuhusu uchaguzi kurudiwa na tulishaandika katika tahariri yetu kutahadharisha kuhusu kauli kama hizo.

Kwa sababu suala la muafaka wa Zanzibar ni muhimu kwa afya ya taifa hili, tunaendelea kusisitiza haja ya kuwapo kwa weledi katika utoaji matamko yanayohusu mazungumzo baina ya CCM na CUF kuhusu mustakabali wa uchaguzi.

Tunazidi kusisitiza kuwa matamko kuhusu kinachoendelea kwenye mazungumzo hayo yatolewe kwa taarifa inayohusisha pande zote mbili ili kujenga imani kwa Wazanzibari kuwa kuna mwelekeo wa kupatikana muafaka.

 

CHANZO: MWANANCHI

 

One Reply to “Wazanzibari wametulia, wanasiasa wasiwachanganye”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.