Maalim vs Seif CCM sita

MAA

Mgogoro huo umeibuka baada ya matokeo ya uchaguzi wa Rais, wawakilishi na madiwani visiwani Zanzibar kufutwa kwa madai ya kuwapo ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi, uamuzi ambao unapingwa na CUF inayodai kuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar alishinda na hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) kumtangaza kuwa mshindi.

 

Dar es Salaam. Wakati jitihada za kutafuta suluhisho la mgogoro wa kisiasa Zanzibar zikiendelea, vikao vinavyoendelea baina ya CCM na CUF havina uwiano wa uwakilishi; makada sita wa CCM dhidi ya Maalim Seif Sharrif Hamad.

Mgogoro huo umeibuka baada ya matokeo ya uchaguzi wa Rais, wawakilishi na madiwani visiwani Zanzibar kufutwa kwa madai ya kuwapo ukiukwaji wa sheria na kanuni za uchaguzi, uamuzi ambao unapingwa na CUF inayodai kuwa mgombea wake wa urais wa Zanzibar alishinda na hivyo kuitaka Tume ya Uchaguzi (ZEC) kumtangaza kuwa mshindi.

Ili kutatua mgogoro huo, pande hizo mbili zimeunda kamati maalumu inayoongozwa na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, lakini inakosa uwiano wa uwakilishi.

Mbali na Dk Shein, wengine walio kwenye kamati hiyo ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Rais wa Serikali ya Awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Serikali ya Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete, na marais wa zamani wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na Dk Salmin Amour.

CUF inawakilishwa na katibu wake mkuu, Maalim Seif ambaye ndiye aliyegombea urais akiungwa mkono na vyama vinne vingine vinne vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) ambavyo ni Chadema, NCCR-Mageuzi, NLD na CUF.

Taarifa iliyotolewa na kaimu mkurugenzi wa Ikulu, Gerson Msigwa Desemba 26 mwaka huu, inaeleza kuwa Dk Shein alikutana na Maalim Sef kujadili suala la Zanzibar akiwa pamoja na marais hao wastaafu.

Kamati hiyo ilianza mazungumzo tangu Novemba 9 kujadili suala hilo la mgogoro wa Zanzibar na hadi sasa mazungumzo hayo bado yanaendelea.

Akizungumzia kukosekana kwa viongozi wengine wa CUF katika vikao mbalimbali, kaimu mkurugenzi wa habari na uhusiano wa CUF, Ismail Jussa alisema hawana hofu ya wingi wa uwakilishi kwa kuwa mazungumzo yameshamalizika.

Alisema kuwa kinachotakiwa sasa ni upande wa pili kukabidhi mamlaka ya Zanzibar kwa CUF, hatua aliyodai haina ubishi. Jussa alisema leo CUF itatoa msimamo wake kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Naye naibu katibu mkuu wa chama hicho, Magdalena Sakaya alisema: “Uamuzi wa kwenda au kutokwenda na mtu ni wa Maalim Seif. Ila ninachopenda kukueleza ni kuwa hata kama Maalim Seif atakwenda na watu 10 au 20, msimamo wa CUF ni ule ule kwamba hatutakubali uchaguzi urudiwe.”

Sakaya alisema katiba ya chama hicho inaeleza wazi kwamba chombo cha mwisho kutoa uamuzi ni Baraza Kuu la Uongozi Taifa, kwamba tayari kikao hicho kimeshafanyika na kutoa msimamo kuhusu Zanzibar.

“Katika kikao hicho, Maalim Seif ndiye katibu na hata katika vikao vingine vya mashauriano na kamati ya utendaji, msimamo ni mmoja kuhusu Zanzibar. Hivyo kitendo cha kuwepo peke yake katika kikao ni jambo la kawaida tu,” alisema.

Alisema CUF ina taarifa za kila jambo linalojadiliwa katika vikao hivyo kuhusu Zanzibar na kusisitiza kuwa msimamo wao ni kutorudiwa kwa uchaguzi huo.

“Hakuna uamuzi mwingine unaoweza kufanyika bila taarifa kuletwa katika kikao na kujadili. Kumbuka kuwa Maalim Seif ni sehemu ya kikao cha Baraza Kuu la Uongozi Taifa,” alisema.

“Tunajua kuwa wanaandaa bao la mkono, na sisi tunajua na hatuko tayari kwa hilo. Anachokifanya Maalim Seif katika vikao hivyo ni kuwaeleza msimamo wa CUF, hakuna kinachoweza kubadilika.”

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alimtetea Maalim Seif kuwa ana uwezo wa kukiwakilisha vizuri chama hicho.

“Maalim Seif ndiye mgombea wa CUF na pia ni kiongozi wa chama. Ana uwezo mkubwa wa kufanya mazungumzo. Hili suala ni letu sote ila linapaswa kutatuliwa zaidi na Zanzibar kuliko Tanzania Bara.”

Mbowe alisema mambo yanayojadiliwa katika vikao hivyo hutolewa taarifa kwa vyama vyote vinavyounda Ukawa, ambavyo navyo hushauri nini kifanyike.

“Ni haki yake kufanya mashauriano mara kwa mara na sisi tunamuunga mkono. Ila kumbuka kuwa kipindi hiki ni cha sikukuu hivyo dharura za viongozi wa Ukawa naweza kuzielewa maana mimi nipo mbali na hata (mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James) Mbatia naye yupo mbali, (Waziri Mkuu wa zamani, Edward) Lowassa naye yuko mbali,” alisema Mbowe.

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, CCM imewataka wafuasi wake kujiandaa na uchaguzi wa marudio ambao ZEC ilisema utafanyika baada ya siku 90.

Wito huo ulitolewa siku tatu zilizopita na Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar iliyokuwa imekutana katika kikao cha kawaida ambacho pamoja na mambo mengine ilifanya tathmini ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na mwenendo wa kisiasa visiwani humo.

Tayari jumuiya za kimataifa na nchi za Ulaya na Marekani zimeshaeleza kuwa uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu na kushangaa sababu za kufutwa kwa matokeo.

 

CHANZO: MWANANCHI

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s