Mishahara ya viongozi yatikisa Zanzibar

Othman Masoud aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
    Othman Masoud Othman aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa SMZ, Othman Masoud Othman, anasema kisheria hata Rais Dk. Shein kuendelea kubaki madarakani si halali hivyo na makamu wake wa kwanza na wa pili wa Rais spika, mawaziri na wajumbe pia uhai wao kikatiba kwa nafasi zao umekoma.

MVUTANO wa kisheria umeibuka visiwani hapa juu ya uhalali wa viongozi wa juu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuendelea kulipwa mshahara. Vigogo wanaoguswa na mvutano huo ni Rais, Makamu wa kwanza na wa pili wa Rais, mawaziri, Spika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi.

Mvutano huo uliowagawa wanasheria katika pande mbili, umeibuka kutokana hatua ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais na wawakilishi.

Upande mmoja wa wanasheria wanasema si halali kwa vigogo hao kuendelea kuchukua mshahara unaotokana na kodi za wananchi na kwamba kwa sasa Zanzibar haina Serikali, huku upande mwingine ukihalalisha kwa madai kuwa ZEC imeufuta uchaguzi huo kwa mujibu wa sheria.

Wanasheria wanaotetea hoja hiyo wanasema kuwa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na vigogo wengine wapo madarakani kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, lakini pia amepewa siku 90 za kuongoza kipindi cha mpito wakisubiri marudio ya uchaguzi, hivyo wanastahili kulipwa mshahara.

Mwanasheria Mkuu wa zamani wa SMZ, Othman Masoud Othman, anasema kisheria hata Rais Dk. Shein kuendelea kubaki madarakani si halali hivyo na makamu wake wa kwanza na wa pili wa Rais spika, mawaziri na wajumbe pia uhai wao kikatiba kwa nafasi zao umekoma.
Masoud anaeleza kuwa uhai wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi ni miaka mitano na kwa sababu baraza halipo na muda wao kuisha hawana haki ya kulipwa mishahara na stahili nyingine.

“Anayepaswa kubeba lawama ya jambo hilo ni muajiri ambaye kama yeye anaamini yupo kihalali wakati yuko madarakani kinyume na Katiba ya Zanzibar, hataweza kuwanyooshea kidole waajiriwa na kuwaambia hawapo na hawastahili kulipwa kwa sababu wote ni wavunja sheria na Katiba, “alisisitiza.

Aliyewahi kuwa Mwanasheria mkuu wa SMZ, Hamid Mbwezeleni anasema kwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi yupo madarakani na bado hajavunja Baraza la Mawaziri hivyo anastahili kulipwa mishahara na stahili nyingine zote.

Mbwezeleni alisema kusita kwa kazi za mawaziri ni pale Rais aliyewateua anapotangaza kuvunja Baraza la Mawaziri au akiamua wakati wowote kumfukuza kazi waziri mhusika.

“Kwanza ninachoamini, Rais Dk. Shein yupo madarakani kihalali kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, wakati wowote anaweza kuitisha Baraza la wawakilishi ikiwa kuna jambo la dharura, “alisema Mwanasheria huyo.

Alisema ikiwa wapo wanasiasa wanaosema Rais hayupo madarakani kikatiba na kwamba hakuna serikali, wanakosea na kama wanaosema hivyo wanatoka upinzani, basi wanapaswa kurudisha magari ya Serikali.
Kwa upande wake mwanasheria wa kujitegemea, Mohamed Ali Ahmed, anapingana na hoja hiyo huku akisema Katiba ya Zanzibar inataja mtu atakayebaki madarakani kwa siku 90 ni Rais na Katiba haitaji uwapo wa makamu wa kwanza na wa pili, mawaziri, spika au wajumbe wa Baraza la wa wakiishi.

Mohamed anasema ukomo wa kazi za mawaziri, spika na wajumbe wa baraza la wawakilishi umegota kikatiba na kisheria hivyo kuendelea kulipwa si haki.

Alisema suala la kuwalipa mishahara watu hao si sahihi kwani uchaguzi umefutwa na utafanyika ndani ya siku 90, hivyo hawastahili chochote.

“Anayeteua mawaziri ni Rais ambaye sasa kuwepo kwake tu madarakani ni ndani ya kipindi cha siku 90 ili uchaguzi mwingine uitishwe, Rais anaweza kuongoza nchi akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mwanasheria Mkuu pamoja makatibu wakuu wa wizara na watendaji wengine bila kuwepo mawaziri na kazi zikaenda kama kawaida ” Mohamed.
Akizungumzia uhalali wa kufutwa kwa uchaguzi mkuu, alijibu kuwa ajuavyo yeye kisheria Mwenyekiti wa ZEC ana madaraka na mamlaka hayo pamoja na mengine bila ukomo.

Hata hivyo Waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amewahi kuthibitisha kuwa mawaziri wote wa SMZ wanaounda Serikali ya Umoja wa Kitaifa, wanaendelea kulipwa mishahara yao na hakuna hata mmoja aliyekataa kulipwa.

 

CHANZO: RAI

 

Advertisements

3 Replies to “Mishahara ya viongozi yatikisa Zanzibar”

  1. Ukinzani Uliopo Kuhusu Uhalali Wa Urais Wa Dr.Shein ,Ni Kupotezeana Wakati Bure Kwa Hoja Za Kishabiki Kama Za Othman Masoud Au Akina Ismail Jussa Na Fatma Karume .Hoja Zao Ni Butu Na Ni Ushabiki Wa Ki-CUF-Zanzibar.

    Kuhusu Wale Mawaziri BANDIA Wa CUF ,Waliojifaragua Kwa Kujitakia Umaarufu Wa Dharura Kwamba Wamejiuzulu -Tuwaulize Ikiwa Walikuwa Wanasema Kweli Mbona Hawakupeleka Barua RASMI Za Kujiuzulu Kwa Rais Na Kwanini Wanapokea Mishahara Minene Bila Ya Kwenda KAZINI ?. Wao Kupokea Mishahara Na Kutojiuzulu Rasmi Kwa Maandishi Ni Ushahidi Tosha Kwamba “Ethics Na Moral Zao Ni Dhaifu Kabisa Na Si Watu Wa Kuaminika “.Wanaburuzwa Na Uimla Wa Wanaowatumia Na Kuwaamrisha Na Wao Wafuata KAMA VIJIBUZI VYA KISIASA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s