Maalim Seif kukabidhiwa mikoba Zanzibar baada ya ‘vutankuvute’?

IMG-20151217-WA0004

Mazungumzo yanayoendelea kwa usiri visiwani Zanzibar na Tanzania Bara kutafuta muafaka kufuatia tangazo la Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu visiwani humo yameendelea kuibua ripoti nzito tofauti.

Taarifa zinazodaiwa kutolewa na mmoja kati ya maziri waandamizi wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimeeleza kuwa vikao viwili vikubwa vilivvyofanyika katika Ikulu ya Dar es Salaam na ile ya Zanzibar Jumamosi na Jumanne wiki hii vimetoa picha inayompa nafasi zaidi Maalim Seif Sharif Hamad kutangazwa mshindi.

Kwa mujibu wa ‘Mawio’, chanzo hicho cha kuaminika, wajumbe wengi wa vikao hivyo wameelezea kuridhia kuwa uchaguzi wa Zanzibar usirudiwe bali aliyeshinda atangazwe ili
kuepusha madhara makubwa yanayoweza kujitokeza.

“Washiriki wengi wa mazungumzo yale wanakubaliana na hoja kwamba kurejea Uchaguzi kutaweza kuingiza nchi katika mgogoro na mkubwa zaidi, “mtoa taarifa anakaririwa
na gazeti hilo.

Aliongeza kuwa Maalim Seif ameendelea kushikilia msimamo wake wa kukataa kurejewa kwa uchaguzi badala yake anataka Tume imalize kazi yake na kumtangaza mshindi.

”Hapa Zanzibar chama chetu kinaonekana kusalimu amri. Hii inatokana na msimamo mkali uliowekwa na CUF katika mazungumzo yanayoendelea pamoja na msimamo wa
Jumuiya za Kimataifa, “anaendelea kukaririwa.

Aliongeza kuwa vikao vya hivi karibuni vilihudhuriwa na Rais John Magufuli, Jaji Joseph Warioba, Dk. Salim na Balozi Madiga.

Hata hivyo, hivi karibuni Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Vuai Ali Vuai aliiambia Azam TV kuwa chama chake kinaendelea kufanya maandalizi ya kurejewa kwa uchaguzi kwa kuwa uchaguzi uliofanyika ulifutwa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali hivyo kufutwa kwa Uchaguzi huo kupo kisheria.

Chanzo: Mawio

Advertisements

2 Replies to “Maalim Seif kukabidhiwa mikoba Zanzibar baada ya ‘vutankuvute’?”

 1. Majadiliano Yapo Kwenye Njia Panda Yenye Ukosi Kwa Ukosi Wa Matamko Mawili
  “Kujitangazia Ushindi Na Kufutwa Kwa Matoeko Ya Uchaguzi “.Wahusika Wa Pande
  Zote Mbili Wamo Kwenye Khofu Ya Kisiasa Ya Kutahayari /Ku-Loose face Usoni Mwa
  Wafuasi Wao/Kichama Na Ulimwenguni

  Kuna mambo 2 yaliyo sugu /worst options,kwa upande wa CUF ,Rudio la uchaguzi
  litawakera wafuasi na washabiki wake – hata endapo Seif Sharif ,atapata Ushindi.
  Msimamo wa CUF – Zanzibar kukataa rudio la uchaguzi ni khofu ya kuporwa ushindi
  na hitimaye kuzuka fujo hatarishi kwa Maisha ya wananchi kwa ujumla .

  Kwa upande wa CCM-Zanzibar- Rudio la Uchaguzi na kushindwa kwa chama huenda likasababisha mpasuko mkubwa Uongozi ndani ya chama na hiyo kusababisha mwanzo
  wa mwisho wa uhai wa chama cha CCM Visiwani.

  Kuna baadhi ya wachambuzi wa kisiasa wanaosikia hili na lile kuhusu yanayojadiliowa
  na wasema kwamba “… huenda pakapatikana upenyo wa `aliyepata apewe `kwa misingi
  ya masharti kwamba sera za CUF Za “Manlaka Kamili/S3 .Kura Ya Maoni Kuhusu Kuwepo Muungano Au La ,zisiwepo kamwe mnamo miaka 25 ijayo “.Kubwa Zaidi Ni Mgawanyo Wa
  Wizara Kwenye Serikali Ya Mseto /SUK Khasa kwenye masuala Ya Usalama ,Ulinzi ,Jeshi
  Na Uhusiano Wa Kimataifa .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s