Disemba 10, 1963 Zanzibar Huriya

Disemba 10, 1963 ndio siku ya Uhuru wa Zanzibar lakini imekuwa haiadhimishwi kabisa
Disemba 10, 1963 ndio siku ya Uhuru wa Zanzibar lakini imekuwa haiadhimishwi kabisa
Tatizo la kuachwa na kupotoshwa kwa historia na kuachwa kusomeshwa vijana maskulini kwamba siku ya Disemba 10 ndio Zanzibar ilipata uhuru wake kutoka kwa Wakoloni, kunachangia kwa kiasi kikubwa vijana kutokuijua historia ya nchi yao na pia kutoshughulika na kuijua siku hii muhimu kwa nchi yao. Na hili halikufanywa kwa bahati mbaya ni jambo la makusudi kusahaulika siku hii na kuadhimishwa siku ya Januari 12 siku ambayo yalifanyika Mapinduzi ambayo kila mwaka huadhimishwa kwa sherehe mbali mbali hapa nchini na kutumia gharama kubwa sana za fedha za umma.

Sio vibaya kuadhimishwa au vijana kusomeshwa kwamba waitambue siku hiyo kwa kuwa ni moja ya tukio muhimu lililowahi kufanyika katika nchi yetu kwa kuwafukuza wakoloni na kuuweka utawala wa Muafrika kama inavyoelezwa lakini na sio vizuri kabisa kuiwacha siku ya Disemba 10 kupita hivi hivi bila ya kumbukumbu yoyote wakati kusingetokea Mapinduzi kama hakukuwa na Uhuru uliopatikana Disemba 10 hapa Zanzibar.
shamte1963
Ni wajibu wetu kukaa na Vijana wetu kuwaeleza historia ya Zanzibar ilipotokea na sio kusomeshwa kuundwa kwa ASP peke yake sio kufanyika Mapinduzi peke yake sio vyama vya ZNP, HIZBU, ZPPP, UMMA na vyenginevyo tu bali historia sahihi inahitajika kusomeshwa ili Vijana wajue wazee wao wametoka wapi, wapo wapi na wapi wanaelekea katika harakati za maisha yao ya kila siku.
3
Vijana wanapaswa wajue kama kupatikana Uhuru wa Zanzibar kuliwahusisha kina nani na nini chimbuko lake hayo yote ni muhimu kwa vijana wetu kuyafahamu yote kwa uwazi na kwa usahihi kabisa.
Ni kosa kubwa kupotoshwa kwa historia yetu ni kosa kubwa kuachwa vijana wasijue tulipotokea na ndio maana tunasema kusiwepo usafi wa mji tu bali kuwepo na usafi wa historia iwekwe wazi kizazi cha leo hakijui tulipotokea hakijui yaliotokea huko nyuma na maisha walioishi mababu na mabibi zao ambao wamepoteza nguvu zao kazi zao umri wao kupigania Zanzibar hadi hapa ilipofikia.
Baada ya maelezo yangu hayo machache naomba usome ushairi huu uliotungwa Sheikh Farouk Abdallah kwa kuiheshimu na kuiadhimisha siku hii  muhimu kwako kwangu na kwa wazanzibari wenzangu ambao tupo katika kupotoshwa tu juu ya historia sahihi ya nchi yetu, tunafichwa na kufungwa fungwa kwenye ukweli juu ya maisha ya wazee wetu.
Kwa Jina la wetu Mola  twaanziya
Twaomba taqwa ikhlasi na hidaya
Sisi waongozwa na waongozi piya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
Twamuhimidi Allah uhuru kurejeya
Na wetu mpenzi Rasuli twamsaliya
Vijijini na mijini sherehe kueneya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Disemba hiyohiyo UNO twaingiya
Dola Zinjibari bendera yapepeya
Dola huru kamili yenye salahiya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Zitwana zijakazi babeenu nisikiya
Machungu neonja na matamu piya
Seona lilinganalo sawa wat’aniya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Amri ya Mola hivyo twesafiriya
Umoja tweuenzi na kuupangiya
Zanzibar yetu sote kuchangiya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
Mwangaza wa kheri kote kueneya
Hakika yabaini mfarakano kufifiya
Wazalendo safu kujenga wat’aniya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
Bahari na mazao  na bandari piya
Uchumi madhubuti nchi kupangiya
Ajira kueneya ombaomba komeya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Wajibu na haqi vyema kusimamiya
Wazee kuenzi ni amri Samawiya
Wanetu amana  sawiya kuwaleya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
Ilimu kuwajengea Akhera na duniya
Wawe wema kwetu na wao dhuriya
Akhera kujijengeya Moto kukimbiya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
Mola twaomba wa’tani kurejeya
Mapenzi na amani ziyada awaliya
Duniya ni njiya Akhera kwendeya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Hizi zetu duwa Mola tutaqabaliya
Sala na salamu kwa Rasuli Nabiya
Mpewa wasila kwetu ni Shafiya
Disemba Kumi Zanzibar huriya
 
Wa Billahi Tawfiiq

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s