EU wazidi kushupalia Uchaguzi Mkuu Zanzibar

Mwangalizi Mkuu wa EU EOM na ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Ulaya, Bibi Judith Sargentini
Mwangalizi Mkuu wa EU EOM na ambaye pia ni mbunge wa Bunge la Ulaya, Bibi Judith Sargentini

Wakati mgogoro wa kisiasa visiwani Zanzibar ukiwa bado haujapatiwa ufumbuzi, Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM), umetoa wito wa ukamilishwaji haraka kwa mchakato wa uchaguzi visiwani humo.

Wito huo umetolewa ikiwa ni wiki mbili zimepita tangu  Serikali ya Marekani kupitia Shirika lake la Millenium Challenge Corporation (MMC), kutishia kutoipa Tanzania msaada wa Sh. trilioni 1.1 hadi pale itakapotatua mgogoro wa kisiasa Zanzibar.

Hii ni mara ya tatu kwa Ujumbe huo wa EU kutoa wito wa kumaliza mgogoro Zanzibar haraka.

Mara ya kwanza ulitoa Oktoba 27, mwaka huu, mara ya pili Oktoba 29 wakati EU, Ujumbe wa waangalizi wa Umoja wa Afrika, Sadc na Jumuiya ya Madola, ilitoa tamko la pamoja kuhusu kumaliza haraka kwa mgogoro huo.

Mwangalizi Mkuu wa EU EOM, Judith Sargentini, alisema jana kuwa EU inafahamu kuhusu mazungumzo yanayoendelea kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF) yanayowashirikisha Marais wastaafu wa Zanzibar ya kutatua mgogoro huo. Alisema EU inarudia wito uliotolewa kwa pamoja na ujumbe mwingine wa uangalizi wa kimataifa Oktoba 29, mwaka huu  unaoishauri Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), kuonyesha uwazi kamili kufuatia uamuzi wa kufuta uchaguzi.

Alieleza kuwa EU EOM imekuwapo nchini tangu Septemba 11, mwaka huu kufuatilia mchakato wa uchaguzi ndani ya Muungano na Zanzibar ikiwa na waangalizi 141.

Alisema waangalizi wa EU EOM nchini walirejea Ulaya katikati ya Novemba, mwaka huu, lakini timu ndogo ya watathmini wa uchaguzi ilibaki nchini kufuatilia ngazi zilizobaki za mchakato wa uchaguzi.

Alisema ingawa mchakato wa uchaguzi Zanzibar haujakamilika, EU EOM itarejea Ulaya kwa muda mwezi huu.

Alisema mbali na jitihada za upatanishi zinazoendelea, EU inaendelea kuunga mkono kikamilifu mchakato wa uchaguzi Zanzibar na kwa mchakato mpana zaidi wa kidemokrasia.

Alisema EU iko tayari kurejea na kuangalia mchakato wa uchaguzi Zanzibar pindi makubaliano ya kuendelea na mchakato huo yanayolingana na chaguzi shirikishi na uwazi zinazotekelezwa kwa wakati na za kuaminika yatakapofikiwa.

Hata hivyo, Sargentini alieleza kuwa EU EOM itawasilisha ripoti kamili ya kina ikiwamo mapendekezo kwa chaguzi zijazo ndani ya miezi mitatu ya kukamilika kwa mchakato wa uchaguzi.

Chanzo: Nipashe

2 Replies to “EU wazidi kushupalia Uchaguzi Mkuu Zanzibar”

  1. Udikteta ni mtazamo wa akili! Kwa miaka 25 hivi, Chama cha Mapinduzi (CCM) kiliendesha mfumo wa kidikteta bila kujali maoni ya raia wake. Waliongopa, waliua, walifilisi, walifisadi, bila wazo la pili. Sasa ni enzi ya vyama-shindani. Hata hivyo, CCM bado ina mtazamo ule ule wa kibabe na kiimla: hata pale mpiga-kura anapokataa kukipa chama hiki mandeiti ya kutawala. Suala sasa ni namna ya kufanya wateule hawa wachache wa CCM wabadili mtazamo wao wa akili kwa manufaa ya jamii. Shinikizo kutoka jamii ya kimataifa liendelee ili, hatimaye, wamiliki wa Chama cha Mapinduzi (CCM) watambue kuwa tunaishi kwenye dunia-asiria isiyovumilia ufisadi wa kisiasa, na kitaasisi. Na wananchi waendelee kuwakumbusha wathibiti wa kampuni hii ya biashara, i.e. Chama cha Mapinduzi (CCM), kwamba nguvu ya ukweli kamwe haififii.

  2. hata kukata shauri wenyeww hayuwezi Mpaka dola za nje ziingikie..Je nn tunaloliweza?
    Uhasama ….na …uadui….hapana…
    Alieshinda apewe aonekane kama anavoonekana Rais Pombe magufuli.
    …….majipu bado babu magufuli una kazi…Nia yako safi kwa Tz….inshaa Alla uwe baba wa Mzizima……DAR SALAAM.(AMEN)

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s