Wanawake 78 wapewa talaka! sababu? ‘kura’

Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa na Sabra Mohammed wakizungumza na waandishi wa habar moja ya mikutano yao kwa wanahabari
Mratibu wa Tamwa Zanzibar, Mzuri Issa na Sabra Mohammed wakizungumza na waandishi wa habar moja ya mikutano yao kwa wanahabari

Women Suffered Divorced Blow in Recent General Elections

Habari kutoka kwa wafuatiliaji wetu sita kutoka Unguja na Pemba zinaeleza kuwa  wanawake 78 ambao 47 wallikatazwa kupiga kura lakini walikwenda na hivyo kupewa talaka, 24 walitishiwa talaka ikiwa watahudhuria mikutano ya kampeni ama watapiga kura matokeo yake wote hawakupiga kura. Wanne waliambiwa wasipige kura na wakapiga lakini hawakuachwa.

USAWA WA KIJINSIA, ZANZIBAR: KESI YA UCHAGUZI MKUU, 2015

Usawa wa kiinsia ni dhamira iliyowekwa miaka mingi na Zanzibar, Tanzania na dunia kwa ujumla. Zanzibar kama ilivyo kwa Tanzania jitihada zake zilianza kuonekana zaidi 1980s baada ya mkutano wa dunia wa wanawake uliofanyika Nairobi, Kenya.

Hata hivyo baada ya miongo mitatu sasa (decade) bado utofauti wa upatikanaji wa haki, maamuzi, kufikia rasilimali baina ya mwanamke na mwaname imekuwa ni kubwa.
Uchaguzi wa hivi karibuni, pamoja na dosari zilizojitokeza, umethibitisha kwa kiasi kikubwa tofauti hiyo ya nguvu. Kwanza katika kinyang’anyiro chenyewe cha kugombea nafasi lakini pia katika upigaji wa kura.
TAMWA kwa kushirikiana na wadau kadhaa ikiwemo UN Women iliweza kutoa  mafunzo kwa wanawake na wanaume vijana 355 kutoka karibu vyama 20 vya siasa.

Na kwa mujibu wa takwimu za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya kisiasa wanawake 30 walisimama kugombea nafasi za uwakilishi kupitia vyama vyao katika ngazi ya uwakilishi, 87 udiwani.

Ni muhimu kufahamu kuwa kati ya hao wanawake  10 wa uwakilishi sawa na asilimia 33.3 na 20 wa udiwani sawa na asilimia 22.9 wamefaidika moja kwa moja na mafunzo yaliyotolewa.
Hata hivyo kama mlivoona waliosimama ni wachache ukilinganisha na idadi ya waliosomeshwa na pia idadi ya wanawake nchini. Hii ilitokana na mifumo iliyokuwemo ambayo haitoi fursa sawa kwa wanawake na wanaume kugombea. Pia, hali ya uchumi mdogo kwa wanawake, rushwa, upotoshaji wa tafsiri ya dini ya kiislamu na utamaduni wa kumlazimisha mwanamke ahusike na kazi za nyumbani tu.
La kusikitisha mpaka mwisho ni kutukanwa matusi makubwa baadhi ya wagombea na wapinzani wao ndani ya vyama.

Kwamfano mgombea ndani ya CCM Kaskazini alikuwa akirushiwa matusi kwenye simu yake ya mkononi hadi alitaka kukata tamaa ya kugombea.

Kwenye upande wa upigaji kura wanawake wengi wamekumbana na udhalilishaji wa kulazimishwa kupigia kura chama Fulani kinyume na ridha ayao.

Habari kutoka kwa wafuatiliaji wetu sita kutoka Unguja na Pemba zinaeleza kuwa  wanawake 78 ambao 47 walikatazwa kupiga kura lakini walikwenda na hivyo kupewa talaka, 24 walitishiwa talaka ikiwa watahudhuria mikutano ya kampeni ama watapiga kura matokeo yake wote hawakupiga kura. Wanne waliambiwa wasipige kura na wakapiga lakini hawakuachwa.

Mmoja katelekezwa baada ya kukataa amri ya kuhudhuria mkutano wa kampeni. Mmoja alifukuzwa na polisi katika kituo cha kupiga kura. Mmoja wao alidai yeye biashara zake hazinunuliwi kutokana na ushabiki wake wa chama cha CCM Pemba.

Baadhi ya kauli za viongozi pia ziliwadhalilisha baadi ya wanwake. Kwa mfano kiongozi mmoja wa juu wa CCM alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kufunga kampenzi za uchaguzi huko Gombani, Pemba alitaja mke wa Kiongozi wa CUF kwamba anaelewa muundo wa sehemu zake za siri.

Tulichojifunza.

Tulichojifunza kwa upande wa siasa ni umuhimu wa kuteua wagombea mapema kupitia vyanzo mbali mbali.
Wawakilishi na wabunge wanaoendelea na mafunzo pia wanahitaji kushiriki katika mafunzo na michakato mbali mbali.

Kwa upande wa ukatili wa kijinsia ni kuhakikisha wanawake wanafikia taarifa zaidi kuhusu haki zao kama wapiga kura lakini pia sera mbali mbali za vyama vya siasa ili kukuza upeo wao wa kujieleza.
Mapendekezo ya kufanya Elimu ya jinsia itolewe kuanzia sasa hadi uchaguzi mkuu ujao.
Mawasiliano yakuzwe baina ya mume na mke hasa kuhusu masuala yanayowahusu.
Elimu ya uraia ipatikane hadi vijijini kwa wanawake na wanaume ili wote wawe na uwelewa unaofanana nahivyo washindane kitaaluma na siyo kitalaka.

Ahsanteni sana.

Mzuri issa Ali P.BOX 741 Tel.0773 747252/0242232263 TAMWA,ZANZIBAR Email:mzurizuri@yahoo.com or zurimzuri@hotmail.com mzuri_issa@tamwa.org

PRESS RELEASE  6-12-2015
Women Suffered Divorced Blow in Recent General Elections
•    Divorced, threats were rule of household management as men break their marriages
Zanzibar_ Lack of civic education and customary patriarchal system remain barrier to married women in Zanzibar to actively participate in democratic process in Zanzibar, and especially during the voting process, observed journalists and media practitioners during a press briefing held TAMWA office at Tunguu on Sunday.
“Married women in Zanzibar were divorced when they voted to a political party not favorable to their husbands”, said Mzuri Issa, a coordinator of TAMWA Zanzibar. Couples divorced just because of voting difference based on party’s affiliation.
From May 2015 towards October 2015, TAMWA carried out trainings to women aspirants aimed to empower them to participate in the entire political/democratic process.
“This efforts seemed to have been run down by men against their wives using marriage to thwart democratic rights of women”, added Mzuri Issa. More than 355women from different registered political parties benefitted from the trainings conducted by TAMWA and the UN Women but only 30 women were nominated by their political parties to run for House of Representatives and councillorship posts.
TAMWA cited North of Unguja and part of Pemba as the most affected areas where divorced were imminently reported as data  shows that 78 women; 47 were simply asked by their husbands not to go to vote but they refused the order and went ahead with their plan hence divorced.
Out of these 78, 24 married women being threatened divorced if they will attend political campaign rallies as a result they didn’t go/attend to the rallies thus denying their democratic rights to participate in politics. The rest were threatened by their husbands and other actors.
Mzuri said the report was conducted by TAMWA through its six mentors from Unguja and Pemba who surveyed the Gender Based Violence acts during and after the election.
Nassra Mohammed who is one of the monitors said that Unguja north A is the most affected District on the divorce saga.
She explained that one of the woman was forced to be visual impaired person so that at the polling station her husband would vote instead of herself.
Asha Abdi Makame, Head of the program providing clarifications to journalists, said that there is an urgent need to intensify civic education to women so that they debate issues instead of being driven by politics of hatred and hostility.

“ The whole issue is about communication between husband and wife and since there was a vacuum of space, then the vice took its own course” she said.

She insisted the dire need of offering civic education to women and men in order to cultivate the culture of respecting each other’s opinion in case of political differences.

According to statistics made available from the Zanzibar Electoral Commission (ZEC), 30 women vied for House of Representatives and 87 as councilors.
The statistics added that among them ten (10) contested to become members of the House of Representatives and 20 were councilors have directly benefited from training provided by TAMWA and UN Women (among the 355 trained).
It has been noted that economic conditions limited to women, corruption, perversion of the religious interpretation of Islam and the culture of the force a woman dealing with the household chores only.
Sadly to say, women aspirants/candidates suffered different forms of abuse or being offended. In one incidence, a woman candidate vying for a seat in north region of Zanzibar received offensive mobile text messages alleged to have originated form male aspirant, her arch rival. The motive behind is simply: to intimidate woman aspirant, harassing her eventually to force her to give up her intention to contest for the post.
Coordinator,
TAMWA,
ZANZIBAR

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s