Mradi wa ufukiaji bahari waanza

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim Baghresa akimueleza Balozi Seif juhudi zinazofanywa na Kampuni yake za kujenga Kisiwa cha Mji Mpya Mtoni Marine.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bakhresa Group Bw. Said Salim Bakhresa akimueleza Balozi Seif juhudi zinazofanywa na Kampuni yake za kujenga Kisiwa cha Mji Mpya Mtoni Marine.

Mradi mkubwa wa Kimataifa wa ujenzi wa kisiwa cha Kitalii  ambacho kitatengezezwa kwa mfumo wa ufukiaji Bahari umeanza rasmi katika eneo la Hoteli ya Utalii iliyopo Mtoni Marine kaskazini Magharibi ya Mji wa Zanzibar.

Hata hivyo gharama kamili za Mradi huo bado hazijafahamika  wakati utakapokamilika  rasmi ujenzi wake hapo baadaye.

Chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini Chenye uwezo wa kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali na kufukia katika eneo linalotengenezwa kisiwa cha Mji Mpya mtoni Marine. Chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini Chenye uwezo wa kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali na kufukia katika eneo linalotengenezwa kisiwa cha Mji Mpya mtoni Marine.
Chombo maalum kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini Chenye uwezo wa kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali na kufukia katika eneo linalotengenezwa kisiwa cha Mji Mpya mtoni Marine.

Mradi huo unaoendeshwa na Kampuni ya Kizalendo  ya Bakhresa Group utahusisha ujenzi wa Hoteli ya Kimataifa ya Ghorofa  Tano ya Daraja la Tano  (Five Star +), utengenezaji wa eneo la wazi la mapumziko (Public Beach) pamoja na kutengeneza  Kisiwa cha Mji mpya .

Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim Baghresa wakishuhudia harakati za kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari kwa chombo maalum hapo Mtoni Marine.
Balozi Seif wa Pili kutoka Kulia akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim Baghresa wakishuhudia harakati za kunyonya na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari kwa chombo maalum hapo Mtoni Marine.

Balozi Seif Ali Iddi alishuhudia harakati za ujazaji wa mchanga katika eneo linalofukiwa ambazo hufanywa kwa utaalamu wa hali ya juu.

Mhandisi wa Mradi huo Ahmed Shamsi alimueleza Balozi Seif  kwamba chombo maalumu kinachotumika kwa kazi ya uchimbaji wa mchanga Baharini  kina uwezo wa kunyonya  na kusafirisha mchanga kutoka ndani ya Bahari sambamba na kukata Majabali.

Sehemu inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadaye kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi kupata mapumziko (Public Beach).
Sehemu inayoendelea kufukiwa hapo Mtoni Marine ambayo itatumika hapo baadaye kwa ajili ya eneo maalum litakalotoa fursa kwa Wananchi kupata mapumziko (Public Beach).

Mhandisi Shamsi alisema kazi hiyo inafanyika kwa saa 12 kila siku ambapo takwimu zinaonyesha wazi kwamba uchimbaji huo wa mchanga unaokwenda  zaidi ya mita 15 chini ya Bahari unafikia  Tani 600 za mchanga kwa saa Moja.

Alifahamisha kwamba harakati za uchimbaji na kufukia mchanga katika eneo hilo zilizoanza Mwezi uliopita wa Novemba zinatarajiwa kukamilika mwezi Januari mwaka ujao.

Balozi Seif akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim wakitembelea kuona mradi wa Ujenzi wa Majengo Mapya ya Hoteli ya Mtoni Marine ambayo iko chini ya Kampuni hiyo kwa hivi sasa.
Balozi Seif akiwa pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Baghresa Group Bwana Said Salim wakitembelea kuona mradi wa Ujenzi wa Majengo Mapya ya Hoteli ya Mtoni Marine ambayo iko chini ya Kampuni hiyo kwa hivi sasa.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bakhresa  Group, Said Salim Bakhresa ambaye ni Mfanyabiashara Maarufu na Mwenyezaji alisema kwamba ujenzi wa mradi huo muhimu kwa uchumi wa Nchi utasaidia mapato ya Taifa pamoja na kutoa ajira kubwa kwa vijana Wazalendo hapa Nchini.

Bakhresa alisema mfumo wa ufukiaji Bahari kwa ajili ya kuanzisha miradi ya Kiuchumi ni mfumo unaotumiwa na Mataifa mbali mbali Duniani ambapo kwa Afrika  mradi kama huo tayari umeanza kutumiwa katika Kisiwa cha Seycheles.

Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Nd. Salum Khamis Nassor akimueleza Balozi Seif hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitege uchumi vyao Nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar  (ZIPA) Nd. Salum Khamis Nassor akimueleza Balozi Seif hatua zinazochukuliwa na Taasisi yake katika kuona taratibu za uwekezaji zinachukuliwa kwa wanaowekeza vitega uchumi vyao Nchini.

Akitoa nasaha zake kwa Balozi Seif ameupongeza Uongozi wa Bakhresa Group kwa uamuzi uliochukuwa wa kuanzisha mradi huo mkubwa wa Kimataifa.

Balozi Seif alieleza kwamba kukamilika kwa mradi huo mkubwa  ambao umeshazoeleka katika Mataifa yaliyoendelea utasaidia kuitangaza Zanzibar na Tanzania kwa ujumla  Kiutalii Kimataifa.

Aidha aliuhakikishia Uongozi huo wa Bakhresa Group kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itatoa kila msaada unaohitajika katika  kuona mradi huo unafikia malengo uliojipangia.

Advertisements

2 Replies to “Mradi wa ufukiaji bahari waanza”

 1. ni nzr ila na wengne kama kina raza wafanye mambo haya na waache kuingia kwenye siasa kwa ajili ya kukimbia kulipa kodi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s