Shein, Maalim Seif wazidi kujichimbia

Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Shariff Hamad
Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein (kushoto) na Makamu wake wa Kwanza, Maalim Seif Shariff Hamad

Mazungumzo ya kutafuta muafaka wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar, yameendelea tena jana Ikulu mjini hapa.
Mazungumzo hayo yaliyowajumuisha viongozi watano wa kitaifa akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na Makamu wa Kwanza wa Rais ,Maalim Seif Sharif Hamad, yalichukuwa takriban saa sita.

Mazungumzo hayo yalianza saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni huku kukiwa hakuna taarifa zozote zilizopatikana kilichofikiwa katika mazungumzo hayo.

Bado vikao hivyo vya mazungumzo vimekuwa na usiri mkubwa licha ya kuenea kwa taarifa zisizo rasmi na ¬†mitaani zimepewa jina la “Dripu”.

Viongozi wengine walihudhuria mazungumzo hayo jana ni Marais wastaafu Amani Abeid Karume, Ali Hassan Mwinyi na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Vikao hivyo vimekuwa na usiri mkubwa ambapo hata viongozi wa vyama vikuu vya siasa vinavyohusika na mgogoro wa uchaguzi Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama Cha Wananchi (CUF), vimeeleza havielewi kilichozungumzwa ndani ya vikao hivyo.

Chanzo cha kuzuka mgogoro huo ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha, kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu  kwa madai kuwa haukuwa wa huru na haki.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

3 Replies to “Shein, Maalim Seif wazidi kujichimbia”

  1. Nadhani mazungumzo ya aina hiyo yanayofanyika mara kwa mara na yanayowajumuisha tu watu hao kwa hao wa upande mmoja tu hayana maana na wala hayafai kuenedelea kufanyika ….Na hii inaonesha wazi ile dhana ya watu wengi kwamba ” wazanzibari bado hawajakomaa kisiasa ‘ na kinachoonekana ni kukomaa kwa “chuki ‘ na itikadi za kichama ” …..Wakati huo huo naelekeza malalamiko yangu kwa kiasi kikubwa kwa vyombo vya kimataifa vilivyosimamia uchaguzi huo huko ZBAR na zaidi UNDP -kwa kushindwa hadi wakati kutatua au kuweza kuingilia suala hilo ili kijulikane kimoja —Hali hii huko Zanzibar inayoendelea ya kuitisha vikao mara leo na kesho halitoweza kabisa kuwasaidia wazanzibar kupata HAKI yao ….vyenginevyo madhara zaidi yataibuka pale watakapoona wazanzibar walio wengi kwa mara nyengine tena wamenyinwa HAKI yao ya KIdemokrasia kwa njia za ulaghai..

    1. The reply is in the ballot itself. Nothing can or should be said beyond this point about the urgency to announce the result of the election, after ultimate completion in counting and sorting of the remaining polls.

      Delaying tactics done by the “Chama Cha Mapinduzi” along with various statements from their so called leaders will do nothing but to arouse more suspicion in respect of the party’s faith and sincerity of the whole election process. To “CCM” election was just a normal practice/exercise intended to show the world that it was done, particularly now that the results were well below their expectation. CCM party needs at least another fifty year’s time to reach to a political maturity, let alone academic maturity. Still asleep CCM will still hold on to the wicked notion that it has to win. Let’s wait and see.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s