CUF waibana Zec Zanzibar

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF Mhe Omar Ali Shehe
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa CUF Mhe Omar Ali Shehe

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kama Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec) wana ushahidi wa kuhujumiwa uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, waonyeshe hadharani wananchi na dunia ipate kufahamu ukweli wake.

Msimamo huo ulitolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe, alipokuwa akizungumzia hatua ya Zec kufuta matokeo ya uchaguzi huo kwa madai ya kubaini vitendo vya udanganyifu.

“Inasikitisha kuona tangu uchaguzi kufutwa matokeo Oktoba 28, mwaka huu,  Mwenyekiti wa tume, Jecha Salim Jecha, ameshindwa kujitokeza hadharani kuonyesha vielelezo na ushahidi wa kuharibika kwa uchaguzi huo,” alisema na kuongeza.

“Tumeishia kuambiwa jumla jumla tu uchaguzi kumefanyika udanganyifu bila ya kuonyeshwa vielelezo na ushahidi wa kuhalibika.”

Shehe alisema tangu kufanyika  uchaguzi huo Oktoba 25, mwaka huu, mpaka sasa hakuna mtendaji yoyote wa Zec aliyefikishwa katika chombo cha sheria kwa kushiriki kuharibu uchaguzi na kusababisha hasara kwa serikali.

Aidha, alisema kama kulikuwa na kura nyingi kuliko idadi ya watu waliosajiliwa katika Daftari la Wapiga, Zec walitakiwa kutaja vituo hivyo na kura zilizoongezeka badala ya kueleza bila ya kuonyesha ushahidi wake.

Alisema kuwa Cuf itahakikisha uchaguzi wa marudio haufanyiki Zanzibar na badala yake Zec wakamilishe kutangaza matokeo ya  uchaguzi wa Oktoba 25 na kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo.

Alisema  pamoja na kuwapo vyama 14 vilivyosimamisha wagombea wa urais wa Zanzibar, lakini vyama vyenye uwakilishi mkubwa wa watu ni CCM na Cuf visiwani humo.

Shehe alisema kama uchaguzi kulitokea kasoro haukupaswa kufutwa wote na badala yake Zec walitakiwa kufanya uhakiki katika maeneo yenye kasoro na kurekebisha.

ZEC YANENA
Mkurugenzi wa Zec, Salum Kassim Ali, alisema uchaguzi wa marudio utafanyika Zanzibar na kwamba kwa sasa taratibu za kufanikisha uchaguzi huo zinaendelea kufanyika.

“Bado ni mapema kutangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio,  lakini wananchi waendelee kuwa na subira baada ya taratibu kukamilika watatangaziwa ili wafahamu na kujitayarisha na uchaguzi huo,” alisema.

CCM YAJIBU
Kwa upande wake, Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kimesema uchaguzi huo utafanyika hata kama Cuf hawatashiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya CCM Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu  CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai, alisema suala la chama cha siasa kushiriki au kutoshiriki uchaguzi ni la hiyari.

Alisema vyama vyenye usajiliwa wa kudumu vipo 22 lakini ni 14 tu ndiyo vilisimamisha wagombea wa nafasi mbali mbali ikiwamo urais katika uchaguzi wa Oktoba, mwaka huu.

Alisema CCM kwa kutambua ukweli kuwa matokeo ya uchaguzi wa awali yamefutwa rasmi, imeanza kufanya maandalizi mazito ya kuingia katika uchaguzi wa marudio.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

2 Replies to “CUF waibana Zec Zanzibar”

  1. Hao ccm wana umwa kweli wakishindwa wao uchaguzi upo huru na salama,Ila wakishindwa wao na wapinzani ndio turudie uchaguzi duuu hii sasa Kali.
    Alikuepo firauni leo yupo wapi kwaiyo ndugu zangu ccm tuelewe kuwa kuna mwanzo na mwisho.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s