Mahakama yamuachia huru Sheikh Ponda

Katibu Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi baada ya mahakama kutoridhishwa na ushahidi wa serikali
Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekuwa akituhumiwa kwa makosa ya uchochezi ameachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro baada ya kutoridhishwa na ushahidi wa serikali

Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Morogoro imemwachia huru kiongozi wa taasisi na
jumuiya za kiislam nchini sheikh ponda issa ponda baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka yaliyofunguliwa mahakamani hapo dhidi yake.

heikh ponda aliachiwa huru na Hakimu mkazi mfawidhi Mary Moyo baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili kutokana na kile kilichoelezwa kuwa dhamana yake ilizuiwa na mkurugenzi wa mashtaka DPP kwa maslahi ya taifa.

Akizungumza mara baada ya kuachiwa huru sheikh Ponda alisema kuwa anaishukuru mahakama kwa kutenda haki japo kuwa imechelewa na kwamba amekaa rumande tangu siku aliyokamatwa kutokana na dhamana yake kuzuiwa.

Katika kesi hiyo iliyovuta watu wengi wakiwemo waumini wa dini ya kiislamu sheikh ponda alikabiliwa na mashtaka mawili ambayo ni kutoa maneno yenye kuumiza imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo alidaiwa kuyatenda agosti 10 mwaka 2013 katika viwanja vya shule ya msingi kiwanja cha ndege manispaa ya morogoro.

Upande wa mashtaka katika kesi hiyo uliwakilishwa na wakili wa serikali mwandamizi Bernard Kongola, Sunday Hyera, na George Mbalassa wakati upande wa utetezi uliongozwa na wakili Juma Nasoro, Abubakar Salim na Batheromeo Tarimo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

3 Replies to “Mahakama yamuachia huru Sheikh Ponda”

  1. Upuuzi wa Mahkama za Nchi yetu zikiendeshwa chini ya mamlaka ya serikali ya CCM huwa inazichelewesha kesi za watuhumiwa …na zaidi kesi zinazowakabili WAISLAAM -hilo linafanyika kwa makusudi kwa lengo la kuwadhalilisha na kuwanyanya Masheikh wa kiislaam. N a bado Mahkama hizo hizo zinathibitisha kuwa Mtuhumiwa hana kosa, Je kwann walimuweka ndani zaidi ya miaka 3 bila ya dhamana ? Je Mahkama za serikali ya CCM itaweza kulipa fidia za mtuhumiwa kwa kupoteza wakati wake na kumkosesha kuendelea kufanya shughuli zake na kuwepo na familia yake? Kama Mahkama hiyo itashindwa kulipa fidia basi tutaelewa kwamba bado serikali ya CCM inaendeleza kile kinachoonekana na wengi ya waislaam “UONEVU DHIDI YA UISLAAM”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s