Viongozi wa dini wataka Shein, Hamad kukubali matokeo ili kuunda SUK

sheinsseifRais Dokta Ali Mohamed Shein na Katibu Mkuu wa  CUF, Seif Shariff Hamad ndiyo waliobeba amani na utulivu wa Zanzibar.
Viongozi hao ambao ni Rais na Makamu wake  wa kwanza, wanahimizwa kutenda haki na kuepuka kuukuza mgogoro wa Zanzibar ambao sasa umeanza kutishia mipango ya maendeleo ya taifa.

Wakuu hawa ndiyo wanaotakiwa kufahamu dhamana hiyo na  wasiwasikilize wapambe ambao mara nyingi hutazama  maslahi binafsi badala ya ustawi wa nchi.

Mgogoro wa Zanzibar wiki hii umetishia kuinyima Tanzania Shilingi trilioni moja (bilioni 999) zinazotolewa na Shirika la Changamoto za Milenia la Marekani (MCC).

Viongozi wa dini wakiwamo,  maaskofu na masheikh kutoka  Tanzania Bara na Visiwani na wa  mataifa wa Maziwa Makuu , wapo Zanzibar kuzungumzia mgogoro huo.

Wanasema  waamini kuwa jibu la amani ya Zanzibar ni Dk Shein na Hamad.

Wanawataka wawili hawa kuutendea haki Uchaguzi Mkuu uliofanyika  Oktoba 25,  2015 na kumtangaza  mshindi wa Urais wa Serikali ya Mapinduzi ya  Zanzibar (SMZ).

Jopo hilo  la viongozi wa kiroho wanaongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili , Amani  na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu, lipo Zanzibar kutathmin mgogoro huo.

Viongozi hao watatembelea majimbo yote ya Pemba na Unguja  huku wakiwahimiza wanasiasa  kuangalia maslahi na ustawi wa Wanzabari badala  ya mambo yanayotishia amani ya taifa.

Wanawakumbusha viongozi suala la Nigeria  ambako mshindwa  alijipambanua  kuwa ameshindwa hata baada ya wapambe kumlazimisha akatae matokeo.

Kama viongozi hao walikiri kushindwa hapo Zanzibar tatizo ni nini ? Mshindi anajulikana au hafahamiki? Katiba inawaagiza iunde Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) basi aliyeshinda aunde serikali hiyo.

Kamati hiyo yenye wataalam wa haki, sheria na utawala bora, imetaka serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar inayomaliza muda wake, kukubali matokeo ya uchaguzi uliopita na kuunda  serikali mpya ya  umoja kwa mujibu wa katiba.

Wanaamini kuwa  kufikiwa hatua hiyo kutaendelea kuin’garisha Zanzibar  badala  ya kuendeleza mivutano ya chuki  inayohamasishwa na chuki za kisiasa  na mambo ya kizamani ambayo yanasambaratisha umoja na mshikamano wa wananchi.

Wanasema  makubaliano yanayoendelea sasa yawe ni kumpa ushindi aliyechomoza na ushindi kwenye Uchaguzi  Mkuu wa Oktoba  ambayo ndiyo kwa upande wa Bara yalimchagua Rais John  Magufuli,  kuwa  Rais wa  Jamhuri ya Muungano.

Akitoa mchango wake  Sheikh Profesa Haduo-Ally Seleman wa  Nigeria,  anaonya kuwa chaguzi nyingi za marudio kwenye nchi  za Afrika ndiyo chanzo cha vurugu kwani kila mgombea hutafuta mbinu chafu za kutaka kushinda.

Anataja mbinu hizo kutumia vitisho vya vyombo vya dola , ahadi hewa,  rushwa na udanganyifu hivyo kuwa chanzo cha vurugu na kukosekana amani.

Profesa  Seleman  anasema maridhiano ya Zanzibar  lazima yalenge  kuwaondoa  watendaji ambao kwa makusudi  waliingiza kasoro zilizoharibu na kuvuruga uchaguzi.

Kwa upande wa serikali, wanatoa wito kuwa Zanzibar kumpa haki mshindi badala ya kurudia uchaguzi kwani hayo ndiyo matakwa ya  kweli ya wananchi kutambua haki yao kwenye boksi la kura.

Kadhalika waliwataka viongozi na  wanasiasa barani Afrika kujifunza  yaliyotokea kwenye Uchaguzi Mkuu  Nigeria pale Rais Good Luck Jonathan aliyeshindwa alipomkabidhi Jenerali Mohamadu  Buhari,  Ikulu bila kelele hata baada ya wapambe  kumshauri akatae matokeo.

Viongozi hao waliopo Unguja na Pemba wataomba dua ya  haki kama nguzo kubwa ya kukuza amani ,uhuru  na ustawi wa jamii kwa wote.

Chanzo: Nipashe

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s