CUF: Hatutaki uchaguzi wa marudio Zanzibar

CUF TibirinziMwinyi Sadallah

Chama cha Wananchi (Cuf) kimesema hakuna mwenye ubavu wa kutengua  maamuzi ya Baraza Kuu la Chama hicho ya kupinga kufutwa matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Ali Omar Shehe, alipokuwa akizungumzia mgogoro wa uchaguzi huo, mjini hapa jana.

Alisema pamoja na mazungumzo yanayoendelea kufanyika ya kutafuta muafaka, lakini msimamo wa Baraza Kuu la Uongozi la Cuf bado uko palepale wa kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) atengue uamuzi wake wa kufuta matokeo ya uchaguzi kurudi kazini kukamilisha kazi ya kutangaza matokeo na mshindi wa uchaguzi huo.

“Baraza Kuu la Uongozi la Cuf lilikutana Zanzibar na kuweka msimamo huo,  hakuna kiongozi yoyote ndani ya Cuf mwenye ubavu wa kwenda kinyume na maamuzi hayo,” alisema. Alisema maamuzi yoyote ambayo yatafanyika lazima yapate baraka za baraza hilo lakini kwa sasa CUF haikubaliani na Zec kutaka kuitisha uchaguzi mpya wisiwani humo.

Msimamo huo wa Cuf umekuja huku kukiwa na tetesi kuwa, mazungumzo kadhaa yaliyofanyika kuhusiana na mgogoro huo na kuwashirikisha viongozi wa ngazi za juu Zanzibar wakiwamo wagombea urais kwenye uchaguzi huo, Rais Mohamed Shein (CCM), Maalim  Sharif Hamad (Cuf) na marais wastaafu imefikia muafaka na kutoka na pendekezo la kurudiwa uchaguzi huo ambalo litawasilishwa katika kila chama kilichokuwa kinashiriki mazungumzo hayo.

Hata hivyo, Msemaji wa Chama cha Mapinduzi Zanzibar, Waride Bakar Jabu, alisema hadi jana chama chake kilikuwa hakijapokea mapendekezo yoyote kutoka katika meza ya mazungumzo hayo alisema yamewaweka njiapanda kwa sababu hawafahamu kinachoendelea. Zec ilifuta matokeo ya uchaguzi mkuu wa Zanzibar Oktoba 28, mwaka huu kwa madai kufanyika vitendo vya udaganyifu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi.

Chanzo: Nipashe

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s