Waziri Mkuu ateuliwa

Waziri Mkuu Mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Majaliwa Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Mteule wa Serikali ya Awamu ya Tano, Majaliwa Kassim Majaliwa.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemteuwa Majaliwa Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tano. Dk Magufuli ametegua kitendawili kilichotanda katika Watanzania wengi hasa wafuatiliaji wa masuala ya siasa.

Kassim Majaliwa ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Ruangwa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jina lake limetajwa muda huu katika Ukumbi wa Bunge Dodoma na Spika wa bunge hilo, Job Ndugai na kuahirisha kikao cha bunge kwa dakika 45 kwa ajili ya kuandaa utaratibu wa Bunge kuthibitisha jina hilo kwa kulipigia kura.

Bahasa iliyobeba jina la Waziri Mkuu imewasilishwa na Mpambe wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika ukumbi wa Bunge huku ikiwa imefungwa kwa bahasha tatu tofauti na ikiwa imeandikwa kwa mkono na Rais mwenyewe hali inayoonesha kulikuwa na usiri mkubwa kuvuja kwa jina la mteuliwa kabla ya kutajwa hapo bungeni.

Kassim Majaliwa kihistoria fupi alizaliwa Desemba 22, mwaka 1960. Majaliwa ndiye aliyekuwa Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa serikali ya Rais Jakaya Kikwete iliyo mpisha Rais Dk. John Magufuli.

Kitaaluma ni Mwalimu aliyepata elimu yake Chuo cha Ualimu Mtwara (Mtwara TTC) na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Kiongozi huyu pia mbali na kufanya kazi katika nafasi mbalimbali serikalini lakini alipitia Jeshi la Kujenga Taifa kambi ya Makutopora (JKT).

Chanzo: Thehabari

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s