Wazanzibari waandamana London

Wawakilishi wa Zawa UK wakiingia 10 Downing Street kukabidhi barua kwa Waziri Mkuu Bwana David Cameroon kuhusiana na sakata la Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Pichani ni Bwana Rashid Ali, Bi Ghariba Said
Wawakilishi wa Zawa UK wakiingia No 10 Downing Street kukabidhi barua kwa Waziri Mkuu Bwana David Cameroon barua ya malalamiko juu ya kutaka mgogoro wa Zanzibar ushughulikiwe haraka. waliokabidhi barua hiyo ni Bw. Rashid Ali, Bi Ghariba Said

Wazanzibari wanaoishi nchini Uingereza leo wamefanya maandamano wakidai haki ya kutangazwa ushindi wa Chama Cha Wananchi (CUF) katika uchaguzi mkuu wa Zanzibar uliofanyika Octoba 25 mwaka huu

 

Maandamano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Zanzibar Welfare Association (ZAWA) ambapo wazanzibari hao wametoka maeneo mbali mbali katika miji yao na kukusanyika katika eneo Downing Street kwenye Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron na uongozi huo kukabidhi barua yao yenye malalamiko kutaka suala la Zanzibar lishughulikiwe.

12247082_455166178000825_8745307794412665492_n

Maandamano hayo yamefanyika kwa lengo la kuongeza shindikizo kwa mamlaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchukua hatua za haraka ya kuhakikisha Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) inakamilisha kazi ya kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.

 

Uchaguzi wa Zanzibar umekwamishwa na uamuzi wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha Octoba 28 alipotangaza kufuta uchaguzi huo wote kwa madai kwamba umekumbwa na matatizo mbali mbali.

12227082_10205370980297892_5516912819446149797_n

Uamuzi huo wa kufuta matokeo umepigwa na Chama Cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) kwa kuwa hauna ngumu kisheria ambapo Mwenyekiti wa tume hiyo hana mamlaka ya kufuta uchaguzi ambao tayari ulishakamilika na matokeo yake kuanza kutangazwa.

9

Wakati jecha akitoa tangazo la kufuta matokeo bila ya kushauriana na tume yake alikuwa tayari ameshatangaza matokeo ya kura za urais za majimbo 31 kati ya 54 ya Zanzibar pia washindi wa nafasi za uwakilishi na udiwani katika majimbo hayo walishatangazwa na walishakabidhiwa vyeti vyao.

12246762_909583235791024_3723168256708153260_n

Barua hiyo iliyowasilishwa na Rashid Ali ambaye kiongozi wa ZAWA wamewasilishwa barua hiyo wakiamini kwamba suala la Zanzibar litashughulikiwa ili wananchi wa Zanzibar waweze kuendelea na maisha yao ya kawaida.

8

Mwakilishi wa ZAWA, Hassan Khamis alisema wameamua kupeleka barua kwenye ofisi za waziri Mkuu wakiamini suala hilo litashughulikiwa ikiwa pamoja na serikali ya Tanzania kuchukua hatua madhubuti na za haraka kaika kushughulikia suala hilo ambalo limewaweka wazanzibari roho juu.

2

“Sisi kama Wazanzibari wameshachoka na hali iliyopo sasa huko nyumbani kwetu ambao kuna jamaa zetu na wazee wetu wanahitaji kuendelea na maisha yao hivyo kuna kila sababu ya kumalizwa mgogoro uliopo ili waendeleaa na maisha yao sasa hivi maisha yamekuwa magumu, vitu havinunuliki khofu imetanda majeshi yamejaa na hali ya khofu ndio imekuwa kubwa kwa wananchi hawajui saa ngapi kutazuka nini” alisema Khamis.

7

Wakizungumza kwa njia ya simu baadhi ya wanawake walioshiriki maandamano hayo wamesema wanaiombea dua Zanzibar ili mgogoro na mkwamo wa kisiasa umalizike ili wananchi waweze kuishi kwa amani kwani suala la kuishi kwa khofu linawatia huzuni hasa wao ambao wapo nje ya nchi.

3

“Tunaumia tukisikia ndugu zetu wa Zanzibar wana mgogoro mwengine uliotokana na uchaguzi kwa sababu ni miaka mingi kulikuwa na hali kama hiyo miaka mitano nyuma kukatafutwa Maridhiano lakini sasa tunarejea nyuma miaka 15 iliyopita, haipendezi na pia inatutia sisi wasiwasi ambao tupo mbali na ndugu zetu” alisema mmoja wa wanawake walioandamana.

6Khamis alisema wamekabidhi barua na imepokewa ambapo wameahidiwa kwamba barua yao itafanyika kazi pamoja na kuonana na baadhi ya viongozi wengine wa serikali ili kupeleka malalamiko yao yafanyiwe kazi haraka.

Wazanzibari hao waliovalia nguo rangi nyekundu na buluu huku wengine wakiwa wamebeba mabango yenye maandishi mbali mbali na picha za Mgombea Urais wa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad wameonekana wakiwa na furaha wakati wa maandamano hayo.

4

Hii ni mara ya kwanza tokea kumalizika kwa uchaguzi wa Zanzibar kufanyika kwa maandamano kama hayo nchini Uingereza ambapo baadhi ya wananchi wanaoishi Marekani nao wameandaa maandamano yao ambayo yanatarajiwa kufanyika wiki ijayo.

5

“ tutafanya maandamano kuitaka Serikali ya Marekani kuingilia kati na kuweka shindikizo kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili mshindi aliyeshinda atangazwe na serikali ya umoja wa kitaifa iundwe wazanzibari washirikiane wajenge nchi yao” alisema mmoja wa wazanzibari anayeishi Marekani.

 

 

5 Replies to “Wazanzibari waandamana London”

  1. haya tushaona iyo comedy mshamfurahisha huyo kibaraka wenu seif kashafurahi haya kalaleni sasa. mpaka mpewe mashinikizo ndo muandamane mbona mmechelewa wapendwa/ mnakumbuka kufunga banda wakati ngombe kashatoka hahaaaaaaa, ule msumari wenu mokuwa mnaimba kwenye kampeni naona umekugandeni wenyewe sasa. haya kachomeni shindano za tetnas msije mkadhurika. kwa nchi hii mnajisumbua tu. mtapata tabu sana nyie kwa ubaguzi wenu yaani hiyo dhambi itaendelea kukuadhibuni mpaka mjue makosa yenu.

  2. mwiteni huko London mumuapishe basi mchoke kuwadanganya hao wajinga wenzenu. kama yeye alikuwa na mamlaka ya kujitangazia ushindi kwa nii asiwe na mamlaka yakujiapisha/ makubwa haya

  3. Muddy usimtukane hayo ni maoni yake kila mmoja awe huru katika kutoa maoni yake kwa mujibu wa upeo wa ufahamu wake jambo la muhimu kama unataka kumfahamisha mtu ukiona kakosea mfahamishe kwa lugha za heshima hata kama yeye hakutumia lugha za heshima katika kutoa maoni, nadhani huo ndio ungwana na tukiwa na utamaduni huo tutakuwa tunajadiliana kwa kuheshimiana bila ya kutukanana. Shukran nyote mlotoa maoni yenu.

  4. Hivi Africa utumwa wa kifikra utaisha lini…nakubali mmeandamana lakini kwa akili zenu zote mmmeenda tena kwa Mkoloni wenu David Cameroon kumkabidhi barua yeye kama nani?…hivi aitawale Uingereza bado haitoshi mnataka arudi tena atutawale na kutuamulia…kwa nini msipeleke malalamiko ofisi za Umoja wa Mataifa zilzopo hapo London…..sio ajabu ndio maana bado mnaendela kubaguliwa hapo London kwa akili za kitumwa kama hizo wote tunaonekana hatuna akili hata za kuamua…vibaraka wa ukoloni kweli nyie bakini huko London waachieni waafrica mambo ya Africa

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s