Shirika la Habari ‘lazima habari’ Z’bar

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, Hassan Mitawi, akielezea jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad, alipotembelea kituo hicho Mnazi mmoja akiwa katika ziara yake ya Kikazi mwaka 2012.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC, Hassan Mitawi, akielezea jambo kwa Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Shariff Hamad, alipotembelea kituo hicho Mnazi mmoja akiwa katika ziara yake ya kikazi mwaka 2012.

SHIRIKA la Utangazaji Zanzibar (ZBC) limezima kwa njia ya kupuuza “khabari muhimu” iliyohusu mkutano wa faragha wa Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na Maalim Seif Shariff Hamad, ambao ni wa kwanza kufanyika kati yao tangu ulipofanyika uchaguzi mkuu Oktoba 25, mwaka huu.

Viongozi hao waliogombania wadhifa wa urais kwa mara nyingine, baada ya kupambana kwa mara ya kwanza uchaguzi mkuu uliopita 2010, wamekutana wakati nchi ikigubikwa na kimya kikubwa tangu ilipoingizwa katika mgogoro wa uchaguzi.

Mgogoro huo ulitokana na tamko la kufutwa kwa uchaguzi nchi nzima lililotolewa na mtu mmoja tu – Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha.

Shirika hilo liitwalo ZBC, ni asasi ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, na linaendesha stesheni ya redio ambayo ikiitwa Sauti ya Tanzania Zanzibar (STZ) na televisheni iliyokuwa ikiitwa (TvZ).

Stesheni ya redio inaitwa ZBC Radio na TvZ inatwa ZBC TV kufuatia mabadiliko ya muundo yaliyofanywa baada ya kuanzishwa shirika hilo kama asasi inayojitegemea, iliyoko chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo.

Kiongozi wa ZBC ni Mkurugenzi Mkuu aitwaye Hassan Abdalla Mitawi, mwanahabari aliyebobea fani ya utayarishaji na usimamizi wa vipindi kwa njia ya televisheni aliyesomea elimu hiyo ya juu nchini Ujerumani.

Anasaidiwa na Naibu Mkurugenzi, Dk. Yussuf Khamis ambaye alisomea kozi ya juu ya uandishi na usimamizi wa televisheni nchini Uingereza. Yeye pia ndiye anayesimamia shughuli za siku kwa siku za ZBC Radio.

Haifahamiki ni kwanini hasa viongozi wa ZBC wamegomea taarifa ya kikao cha viongozi wakuu wa vyama vinavyoshindania mamlaka ya kuongoza Zanzibar, ambao wanaangaliwa kwa jicho kali kama ndio “watatuzi halisi” wa mgogoro huo.

Mitawi yuko karibu kiuhusiano na serikali na maofisa wa Ikulu na watendaji wa Wizara ya Habari na Tume ya Utangazaji Zanzibar (ZBC), uhusiano unaoonekana hauwezeshi ZBC kukosa habari muhimu kama hiyo ya mkutano wa viongozi hao.

Wakati Dk. Shein anataka kuongoza kwa muhula mwingine wa miaka mitano, Maalim Seif anauhakika ameshinda uchaguzi huu lakini anafanyiwa “mizengwe” na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Viongozi wa CCM wamekuwa wakitamka hadharani siku zote kwamba “Serikali iliyopatikana kwa mapinduzi, haiwezi kutolewa kwa vikaratasi.”

Maana yake ni kwamba kwa kuwa serikali ilitokana na mapinduzi ya Januari 12, viongozi wa CUF wakiitaka, “basi nao wapindue.”

Ni kauli ambayo wachambuzi wa masuala ya siasa, haki za binaadamu na wanasheria wanaichukulia kama “siasa chafu za kihafidhina” zilizolenga kuzorotesha ukuaji wa demokrasia nchini.

Kidunia, uchaguzi wa viongozi kidemokrasia, unachukuliwa kama njia muafaka ya kuipatia nchi yoyote uongozi unaotokana na ridhaa ya wananchi na kudumisha utaratibu wa kidemokrasia wa kukabidhiana madaraka kwa amani.

Kwa sababu hiyo, inaonekana kwamba kufichwa kwa habari iliyohusu kukutana kwa Dk. Shein na Maalim Seif, ni pigo kwa jitihada za viongozi hao wahafidhina wa CCM kupigania kuhujumu ushindi wa Maalim Seif ambaye amekuwa akilalamika kuwa anaporwa ushindi ili kuzuia mabadiliko ya uongozi Zanzibar. Amelalamikia uchaguzi wote tangu ule wa kwanza chini ya mfumo wa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s