SUK itumike kuinusuru Zanzibar

Aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume akisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad pembeni ni Ismail Jussa Ladhu. wakati wakitafuta suluhu na mgogoro wa kisiasa Zanzibar Novemba 5, 2009.
Aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume akisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad pembeni ni Ismail Jussa Ladhu. wakati wakitafuta suluhu na mgogoro wa kisiasa Zanzibar Novemba 5, 2009.

Salma Saidi

Zanzibar: Umoja wa Vijana wa Chama Cha Wananchi (JUVICUF) imeomba muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) utumike katika njia moja wapo ya kuendelea kuinusuru Zanzibar ili isiingie katika machafuko.

 

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao Vuga Mjini Unguja, Katibu Mtendaji wa Umoja huo, Mahmoud Mahinda alisema hivi sasa Zanzibar imo katika mkwamo wa kisiasa na kikatiba hivyo kuna kila sababu kutafutwa ufumbuzi wa haraka ili nchi isiingie katika kusikotarajiwa.

 

“Maamuzi ya Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Zanzibar yanaweza kabisa kuitia nchi katika dimbwi la mivutano na kuirudisha nchi katika siasa za uhasama ” alisema Mahinda.

 

Aidha Jumuiya hiyo imeiomba Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ambayo ilisitisha zoezi lake la kuhesabu kura na kulifuta kabisa kurudi tena kazini pale ilipoishia na kutangaza matokeo ya uchaguzi uliomalizika kwa njia zote za uwazi na halali.

 

“Tume wamalize kutangaza matokeo pia itoe tamko kwa mtu aliyeshinda uchaguzi wetu wa Octoba 25, mtu aliyeshinda nafasi hiyo aapishwe kuwa urais kama matakwa ya sheria na katiba yalivyo ” alisema Mahinda.

 

Aidha alisema kwmaba mtu aliyeshindwa akubali matokeo na kuruhusu nchi isonge mbele na sio kuitia katika mkwamo kama ilivyo sasa ambapo wananchi hawajui kinachoendelea katika nchi yako na hali ya wasiwasi imezidi kutawala nyoyo za wazanzibari wa ndani na nje ya nchi.

 

“Tunaomba CCM iondokane na kalbi kassi (nyoyo ngumu) na mawazo mgando kuwa ni chama hicho tu ndicho chenye haki ya kutawala nchi hii” aliongeza.

 

Akizunggumzia athari ambazo zimetokana na kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi  Octoba 28 baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salum Jecha, Mahinda amesema kitendo hicho kimeleta atahri kubwa kisheria, kisiasa na kikatiba.

“Uamuzi wa Jecha umeitia nchi hadi sasa katika ombwe na ombwe hilo linaweza kuendelea maana hakuna njia ya kikatiba ya mtu yoyotekushika madaraka ya urais baada ya muda wa Dk Shein kumalizika ” alisema Mahinda.

 

Alisema kwamba hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kukaimu mamlaka ya nafasi hiyo muhimu na kwa maana kwamba Zanzibar inaingia katika kipindi kisicho na dira kwa maamuzi hayo ya Mwenyekiti wa ZEC.

 

Umoja huo uliwaambia waandishi wa habari kwamba licha ya taarifa kutoka serikalini na kwenye CCM kutaka kurejea uchaguzi upya wao hawaoni sababu yoyote ya kurejea uchaguzi tena kwa kuwa hakuna sababu za kisheria kufutwa kwake na hakukuwa na mamlaka ya kisheria kuufuta.

“Kitendo hicho cha kufuta matokeo ya uchaguzi kimedhihirisha mkono wa CCM katika maamuzi ya tume baada ya kila dalili kuonesha kuwa ilikuwa inakwenda na maji” alisema Katibu huyo.

 

Umoja huo umesema licha ya kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza katika uchaguzi uliofanyika Octoba 25 lakini uchaguzi huo ulikwenda kwa salama na Amani na kuthibitishwa na waangalizi wa ndnai na nje.

 

“Kasoro zote zilizotokea ziliridhiwa na tume kutamka kuwa uchaguzi umekwenda vyema na kwamba utaratibu wa kuheshimu kura ulifanyika kwa ukamilifu wake na hakuna malalamiko yalioifanya tume kutoa matamshi yoyote kinyume na kuridhia” alisema kiongozi huyo.

 

Mahinda alisema kwamba matokeo ya uwakilishi na udiwani yalipitishwa katika majimbo yote 54 na hapakuwa na malalamiko ya wazi ya aina yoyote yaliokuwa yamefikishwa kwa tume.

 

Aidha alisema vyama vyote vya siasa vilikuwa vimeridhia matokeo ya uwakilishi na udiwani na kila chama kujua ilichopata na kutia mfukoni.

 

“Tume ilikuwa imepokea matokeo yote na kuyathibitisha kidogo kidogo na kufika kutangaza matokeo hayo kufikia majimbo 31” alisema Mahinda.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s