Bidhaa bei juu Zanzibar

Bidhaa mbali mbali ikiwemo vyakula zimepanda bei kufuatia hali tete iliyopo katika visiwa vya Zanzibar
Bidhaa mbali mbali ikiwemo vyakula zimepanda bei kufuatia hali tete iliyopo katika visiwa vya Zanzibar

Salma Said

Zanzibar: Hali ya uchumi Zanzibar inazidi kudororo huku bei za bidhaa zikizidi kupanda kutokana na meli zinazosafirisha bidhaa hizo kutoka Tanzania Bara kupunguza safari zake kutokana na mkwamo wa kisiasa uliopo hapa Zanzibar.

 

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wafanyabishara katika masoko makuu ya Darajani na Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharibi wamesema wanalazimika kupandisha bei kutokana na ughali wa bidhaa kupandishwa bei.

 

“Gunia la viazi mbatata tulikuwa tu7kinunua shilingi laki moja lakini sasa tunanunua kwa shilingi laki mbili na nusu unategemea tutauza kiasi gani lazima tuuze kilo moja shilingi kilo elfu 1.500 au elfu mbili badala ya mia nane” alisema Abdi Sulaiman.

 

Nasoor Khalid naye anasema bidhaa kama maharage, kunde, mbaazi hivyo husafirishwa kutoka Tanzania Bara lakini wamekuwa hawavipati kutokana na safari za meli kupuinguza safari zake jambo ambalo linawasumbua wanunuzi wa bidhaa hizo.

“Bidhaa zangu zinatoka Mbea, Arusha na Ifakara lakini hadi zifike Zanzibar inachukua siku mbili au tatu lakini tokea kumalizika uchaguzi imekuwa ngumu kupata bidhaa hizo afadhali bidhaa za nafaka hununuliwa sana Mwezi wa Ramadhani kwa hivyo afadhali kidogo wanaohitaji sio wengi kwa sasa” aliongea Khalid.

 

Kwa upande wa wauzaji wa viteweo kama nyama, samaki, dagaa na mbogamboga za majani nazo hazijasalimika katika upandaji wa bidhaa hizo ambapo zimekuwa na ugumu wa upatikanaji wake kutokana na baadhi ya mbogamboga hutoka Tanzania Bara.

 

Mbogamboga za majani kama Mabamia, Mchicha, Kabechi, Nyanya (Tungule) Vitunguu saumu na vitunguu maji na nazo zimeadimika katika masoko ya Zanzibar kufuatia kupunguzwa kuletwa kutoka Tanzania Bara hivyo bidhaa hizo zimepanda bei sana kutokana na uhaba wake.

 

“Tungule kilo ilikuwa 1.500 lakini sasa kilo moja 3.000, nyama kilo moja 12.000 badala ya bei yake ya kawaida 8.000 kwa kweli bidhaa zimepanda bei sana na wananchi hawawezi kununua hizo bidhaa” alisema Mohammed Suleiman ambaye ni muuza Nyama katika Soko Kuu la Darajani.

hqdefault

Kwa upande wa wauzaji wa Soko la Mwanakwerekwe ambao baadhi ya bidhaa huchukua mashamba wanasema wanalazimika kupandisha bei kutokana na hali ya usalama kuwa tete kila mtu anaogopa kuleta bidhaa zake Mjini ingawa wanajua zinaweza kununuliwa na kumalizika lakini khofu ya usalama ianwatia wasiwasi.

 

“Sio kwamba hatutaki kuleta viti kuuza Mjini lakini hali haijatengemaa njia kila wakati zinafungwa majiani lakini pia hizo gari zinazozunguka za vikosi na kupiga mabomu ya machozi kila pahala nayo ni mambo yenye kuturejesha nyuma” alisema Nyange Makame mletaji bidhaa kutoka Kaskazini Unguja.

 

Bidhaa kama Ndizi, Mihogo na Mabungo ambayo huletwa kutoka Kisiwani Pemba  nazo zimeadimika kutokana na waletaji wa bidhaa wamepunguza kuleta bidhaa zao Kisiwani Unguja kutokana na hali tete.

 

“Ndizi moja shilingi 1.000 hadi 1.500 na wakati mwengine unapata 5 unaweza kupata kwa shilingi 15 na ndizi zenyewe ndogo kabisa” alisema mnunuzi Asha Abdulrahman.

 

Fatma Said Mohammed anasema wanaogopa kwenda kununua bidhaa kutokana na hali ilivyo kwani wanahitaji bidhaa lakini kutokana na hali ya wahka wanaogopa kwenda madukani na kununua vitu.

 

“Bidhaa zimepanda bei sana lakini pia kuna tatizo hili la kiusalama kuna hali ya khofu kila mmoja amepatwa na khofu anaogopa kutoka vyakula vyetu vishamaliza majumbani lakini mtu anaogopa kutoka nje na wakenda wananunua na kukimbia haraka kurudi nyumbani huko kila wakati Darajani mara magari ya jeshi mara mapolisi khofu tupu” amesema Fatma.

 

Wananchi mbali mbali waliozungumza na Gazeti hili wanaiomba serikali kumaliza suala la uchaguzi na kurejesha hali ya usalama Zanzibar ili wananchi wapate kurudi katika hali zao za kawaida kwani kutokana na maisha yalivyopanda hawawezi kuhimili hali hii ya uchumi.

 

 

 

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s