Maalim Seif: Wazanzibari endeleeni kuwa watulivu

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishin wa Habari katika ofisi za CUF Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishin wa Habari katika ofisi za CUF Mtendeni kuhusiana na maendeleo ya “mkwamo” wa kisiasa Zanzibar

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amesema jitihada za kuutafutia ufumbuzi mkwamo wa kisiasa Zanzibar uliotokana na tamko la Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Bw. Jecha Salim Jecha baada ya kutangaza kufuta uchaguzi uliofanyika tarehe 25 Oktoba 2015, zinaendelea vizuri.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za CUF Mtendeni mjini Zanzibar, Maalim Seif ambaye pia ni mgombea Urais kupitia Chama hicho amesema ana matumaini kuwa suala hilo litapatiwa ufumbuzi wa haki unaoheshimu maamuzi ya wapiga wa Zanzibar waliyoyafanya tarehe 25 mwezi uliopita.

Amefahamisha kuwa jitihada hizo zimekuwa zikifanywa na taasisi mbali mbali za ndani na nje ya nchi zikiwemo Umoja wa Mataifa pamoja na nchi kadhaa ambazo ni marafiki wa Tanzania zikiwemo zilizoleta waangalizi wa kimataifa katika uchaguzi huo.

Amesema jitihada pia zimekuwa zikifanywa na viongozi wakuu wastaafu, viongozi wa dini na Msajili wa vyama vya siasa Tanzania Jaji Francis Mutungi.

Ameeleza kuwa Chama Cha Wananchi CUF kimetiwa moyo na imani kutokana na jitihada hizo, na kwamba ufumbuzi wa haki wa suala hilo utapatikana katika kipindi kifupi kijacho.

Maalim Seif ametumia firsa hiyo kuwataka Wazanzibari waendelee kubaki watulivu na kuitunza amani ya nchi, na kuwaaachia viongozi wao kulifanyia kazi suala hilo kwa kushirikiana na watu mashuhuri pamoja na Taasisi za kitaifa na kimataifa.

Amewaomba wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kufanya juhudi kuhakikisha Zanzibar inabaki katika hali ya amani na utulivu, na kutokubali kutumiwa na wanasiasa kufanikisha mbinu chafu ambazo zinaleta taharuki na hofu miongoni mwa raia.

Maalim Seif amewahakikishia viongozi na wanachama wa CCM na Wazanzibari wote kwamba iwapo atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hakutokuwa na ulipizaji wa kisasi, na kwamba atafanya kazi kwa ushirikiano chini ya muundo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa maslahi ya Zanzibar.

Chanzo: OMKR

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s