Tamko kutoka Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania

Embassy_logo_300x234

28 Oktoba, 2015

Ubalozi wa Marekani unafuatilia kwa karibu mchakato wa uchaguzi nchini kote Tanzania. Tunaendelea kufuatilia zoezi la majumuisho ya kura, ikiwa ni pamoja na zoezi linaloendelea la  majumuisho ya kura za urais wa Zanzibar linalofanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Tunatoa wito kwa mchakato huu kukamilishwa kwa wakati na kwa uwazi. Aidha, tunatoa wito kwa maafisa wote wa serikali kuheshimu wajibu wa waangalizi rasmi wa uchaguzi kwa kuwaruhusu bila kipingamizi chochote kuangalia vipengele vyote vya mchakato wa uchaguzi. Tunazisihi pande zote husika kuhakikisha kuwa mchakato wa uchaguzi unakuwa wa uwazi, huru na wa amani.

Source: Press Release US Embassy Tanzania

One Reply to “Tamko kutoka Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania”

  1. serikali ya USA ndio nchi ya mwanzo inayoongoza kwa kuleta VURUGU na VITA duniani …..mafuriko ya vita kuanzia huko Afghanistan/ Iraq/ Syria / Libya / Haiti / Venezuala / Congo/ Mali / hadi huko YEMEN yamesababishwa na Marekani ….kwa kusaidia pia vikundi vya kigaidi vilevile; Nchi kama TZ haihitaji watu ambao nao wamejaa damu za watu kuja kujifanya wao ndio WASIMAMIZI au WAPATANISHI …..Mbona wameshidwa miaka yote hiyo kuingilia kadhiya ya PALESTINA angalau Ardhi ya waPalestina iliochukuliwa kwa mabavu na ISRAEL irejeshwe kwa raia wa PALESTINA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s