Maalim Seif: Natarajia ushindi wa zaidi ya asilimia 70

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, amepiga kura katika kituo cha Garagara Shehia ya Mtoni Kidatu jimbo la Mtopepo.

Maalim Seif ambaye pia ni Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Wananchi CUF, amepiga kura katika kituo hicho mnamo majira ya saa nne asubuhi.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupiga kura, Maalim Seif amesema ameridhishwa na jinsi wananchi walivyojitokeza kupiga kura, sambamba na utulivu uliokuwepo katika kituo hicho.

Ameelezea matumaini yake ya kupata ushindi katika uchaguzi huo, na kwamba iwapo uchaguzi utafanyika katika hali ya uhuru, haki na uwazi atakubaliana na matokeo ya uchaguzi huo.

“Sina wasi wasi na ushindi na matarajio yangu ni kupata ushindi wa zaidi ya asilimia 70”, Maalim Seif amewaambia waandishi wa habari.

Hata hivyo amesema tayari zimeripotiwa baadhi ya dosari ikiwa ni pamoja na tuhuma za kuwepo kwa masunduku ya kura feki katika kituo cha skuli ya Jang’ombe.

Amesisitiza haja ya kuwepo kwa uchaguzi huru na wa haki, ili kutoa fursa kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwasili katika kituo cha kupigia kura cha Garagara kwa ajili ya kupiga kura

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhiwa karatasi za kupigia kura tayari kwa kwenda kupiga kura

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura kwenye sanduku la kura
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitumbukiza karatasi ya kupigia kura kwenye sanduku la kura
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika kituo cha Garagara jimbo la Mtopepo
Hichi ndicho kituo ambacho Maalim Seif amepiga kura. (Picha na OMKR)

Chanzo: OMKR

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s