Sala ya kuiombea nchi amani

Sala na dua ya pamoja iliyosaliwa jana kwenye uwanja wa Lumumba na kuongozwa na Sheikh Omar Khalfan
Sala na dua ya pamoja iliyosaliwa jana kwenye uwanja wa Lumumba na kuongozwa na Sheikh Omar Khalfan

Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) zimefanya sala na dua ya pamoja leo kwa lengo la kumuelekea Mwenyeenzi Mungu ili awavushe salama watanzania wote katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika keshokutwa nchi nzima Tanzania Bara na Zanzibar.

Sala hiyo imefanyika katika viwanja vya Lumumba nje kidogo na mji wa Zanzibar iliongozwa Sheikh Ali Abdallah Shamte na kisha kufuatiwa na dua iliyosomwa na Sheikh Omar khalfan ambayo ilianzia na kutajwa kwa jina la Mwenyeenzi Mungu Mkubwa.

baada ya takbir hiyo Sheikh Khamis Yussuf akaanza kuelezea umuhimu wa kumuelekea mwenyeenzi Mungu hasa katika kipindi hiki amabcho amesema lengo la dua hiyo ni kumuomba Mwenyeenzi Mungu aivushe nchi katika balaa na madhila ambayo yanaweza kutokea wakati wa uchaguzi.

Amesema dua ni muhimu kwani Mtume Muhammad s.aw ameomba na ametakiwa kuomba dua na wanaadam wanatakiwa katika jambo lolote la kheri kumuelekea Mwenyeenzi Mungu ili awasaidie katika dhida hivyo kusoma dua ni jambo muhimu na linalokubalika katika uislamu.

Sheikh Yussuf amesema dua na sala hiyo haijakusudia kukiangusha chama Fulani kushinda au kushindwa bali ni kwa sababu ya kuiombea nchi isiingie katika balaa katika kipindi chote cha uchaguzi hadi kumalizika kwa kutangazwa matokeo kwani uzoefu uonaonesha

Hata hivyo waumini hao hawakujazama kwa wingi nilitaka kujua ni kwa nini watu hawakuwa wengi kama ilivyotarajiwa? Halima Kassim Muhammad ni mjumbe wa jumuiya ya wanawake wa kiislamu anaelezea sababu zilizochangia kukosekana watu wengi.

Amesema moja ya sababu kuu ni kwamba mawakala wa JUMAZA waliootwa na tume ya uchaguzi ambapo Jumaza imesimamisha mawakala wapatao 182 na hivyo kuitwa kwao na tume kumechangia kushindwa kufika kwneye dua hiyo.

Alisema jambo jengine ni mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vyaKibanda Maiti Mkoa wa mjini Magharibi ambapo baadhi ya watu wameona ni muhimu kwenda kwenye mikutano wamehudhuria mikutano na walioona umuhimu wa dua wamekwenda kwenye dua hiyo.

Katibu Mtendaji wa jumuiya ya maimau Zanzibar Sheikh Muhidin Zubeir Muhidin amesema uzoefu unaonesha kuwa tukio la uchaguzi hufuatiliwa na uvunjifu wa Amani, machafuko na vurugu, hasama na vitendo viovu ambavyo hugharimu maisha ya wananchi na miondombinu ya serikali hivyo wanamuomba Mwenyeenzi Mungu awaepushe na balaa hilo.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s