Dua Maalum ya kuombea uchaguzi

duaaZanzibar: Jumuiya ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA) leo (ijumaa) imeandaa dua maalum ya kitaifa ya  kuiombea nchi kuwa katika hali ya amani na utulivu katika kupindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Dua hiyo ambayo pia itazishirikisha tasisi nyengine za kidini nchini humu inatarajiwa kufanyika katika viwanja vya Lumumba Mjini Unguja wakati wa saa 10:00 za jioni alasir.
Akizungumza na waandishi wa Habari Katibu Mtendaji wa (JUMAZA) Muhiddin Zubeir Muhiddin, huko ofisini kwake Mkunazini Mjini Unguja, alisema kuwa matayarisho ya dua hiyo tayari yameshakamilika.
Alisema kuwa lengo kuu la dua hiyo ni kuiombea nchi kuwa katika hali ya amani wakati wa Uchaguzi na baada ya Uchaguzi ,huku akisisitiza kuwa maisha baada ya Uchaguzi yapo.
Katibu huyo alisema kuwa kutokana na historia ya Uchaguzi hasa Zanzibar inaonesha kuwa mara nyingi huambatana na vitendo vya uvunjifu wa amani, ikiwamo Vurugu, uhasama vitendo ambavyo hupelekea hugharimu mali za watu pamoja na kuondoka kwa mshikamano katika jamii.
Alifahamisha kuwa hali kama hizi ni wazi kuwa zimeweza kujitokeza katika Chaguzi zilizopita hapa Zanzibar ukiachilia ule wa mwaka 2010, ambao ulitokana na maridhiano ya Wazanzibar.
“Kutokana na historia yetu hapa Zanzibar pamoja na kauli za wanasiasa zinazoendelea kutolewa na baadhi ya viongozi wa kisiasa, Taasisi za kiislamu visiwani humu tumepata hofu ya mustakabali wa nchi yetu, ndio maana tumeandaa dua hii maalum ya kuiombea nchi yetu Amani”alisema katibu huyo.
Katibu huyo alisema kuwa dua hiyo imendaliwa na Jumuiya yao kwa kushirikiana na taasisi nyengine za kidini na wala hakuna mkono wa Serikali wala Chama cha Siasa ambacho kimeshirikiana nacho katika kufanikisha maombi hayo.
“Nataka kuweza wazi kuwa Dua hii haitokani na matakwa ya Chama chochote cha Siasa wala Baraka za kiongozi wa kisiasa bali inatokana na matakwa ya Waislamu wote walioamua kumuelekea Mola wao kuomba Amani na Salama”alisema Katibu huyo.
Hivyo katibu huyo aliwaomba Waislamu nchini kujitokeza kwa wingi katika viwanja vya Lumumba Mjini Unguja, ili kuunga mkono jitihada za Taasisi za dini katika kuiombea dua nchi kufanikisha harakati za Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo zifanyike katika hali ya Amani na Usalama.
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s