Maalim awataka Dk Shein, Balozi Idd wadhibiti vurugu

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa dini ya Kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano kilichopo Welezo
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na viongozi wa dini ya Kikristo waliopo Zanzibar katika kituo cha utengamano kilichopo Welezo

Zanzibar. Mgombea urais wa CUF, Zanzibar chini ya mwamvuli wa Ukawa, Maalim Seif amesema amewataka Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ally Idd kuhakikisha wanadhibiti vurugu zinazoweza kutokea katika uchaguzi mkuu ujao la sivyo watapelekwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC).

Maalim Seif alisema hayo, katika viwanja vya Fumba, jimbo la Dimani mkoa wa Mjini Magharibi wakati akihutubia mkutano wa kampeni jana.

Alisema kumekuwa na vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani ikiwamo kusambaza sare za CUF ambazo vijana wa CCM, wamekuwa wakizutumia kufanya vurugu.

Alisema kitendo hicho kinaifanya CUF kuonekana kama mashabiki wake, ndiyo wanaofanya vurugu jambo ambalo siyo sahihi.

Maalim alisema mbinu zote zinazofanywa na CCM, yeye na viongozi wenzake CUF wanazitambua na kuwa wamekuwa wakizipata baada ya muda mfupi.

Aliwataka wananchi na wanachama wa chama hicho, kukichagua chama chake ili kipate nafasi ya kuongoza katika kipindi kijacho cha miaka mitano. “Katiba iliyopitishwa na CCM inayo mambo ambayo yanakisaidia chama hicho na ikiwa nitaingia madarakani mchakato huo utaanza upya ili kuweka mambo yatakayowafaa Wazanzibar na siyo CCM peke yao.”

Naibu wa katibu mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Mazrui alisema kuwa wakati umefika kwa Wazanzibar kuichagua CUF kwa madai kuwa tangu CCM iongoze, maendeleo yalisimama.

Alisema Wazanzibari wanaotaka maendeleo kamili wawashawishi wenzao, kuipigia kura CUF ili wasiendelee kuburuzwa na Serikali ya Muungano.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s