Piga kura rudi nyumbani – Mzirai

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar,kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya Baraza la vyama vya Siasa Constantine Akitanda na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa ya Baraa la vyama vya Siasa John Lifa Chipaka.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Peter Kuga Mziray akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya uchaguzi katika Ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Zanzibar,kulia ni Mwenyekiti wa kamati ya Fedha ya Baraza la vyama vya Siasa Constantine Akitanda na kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge na Siasa ya Baraa la vyama vya Siasa John Lifa Chipaka.

Baraza la Vyama Vya Siasa nchini limevitaka Vyama vya Siasa kuwaasa wagombea wao kurudi nyumbani baada ya kupiga kura na kukubali matokeo yatakayotolewa na Tume za Uchaguzi katika Uchaguzi Mkuu unaoratajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu

Akisoma makubaliano yaliofikiwa na Vyama vyote vya Siasa Mwenyekiti wa Baraza hilo Peter Kuga Mzirai mbele ya waandishi wa habari huko katika ukumbi wa Hoteli ya Bwawani Mjini Unguja jana, alisema kuwa kila chama kinapaswa kukubali matokeo hayo kutokana na makubaliano walioafikiana katika vikao vyao.

Alisema kuwa katika makubaliano hayo kila Chama pamoja na wadau wa siasa walikuwa na fursa ya kutoa maoni yao juu ya harakati zote za kufanyika kwa  Uchaguzi hadi kufikia mda wa kutangazwa matokeo na watendaji wa Tume ya Uchaguzi hivyo ipo haja kwa wajumbe hao kuheshimu makubaliano walioafikiana.

Hata hivyo Mzirai alisema kuwa pindi mgombea yoyote ambae atakuwa hakuridhika na matokeo yatakayotangwa na Tume ya Uchaguzi ana haki ya kulalamika au kukata rufaa ikiwa atakuwa na fomu maalum ambazo zitatolewa kwa Mawakala wa Vyama vya Siasa mara baada ya kumalizika kwa hesabu katika kila kituo cha kupigia kura.

“Mwaka huu kumeandaliwa fomu maalum katika majimbo yote 264, ambayo itakuwa na namba 24’A’ambayo pindi mgombea yeyote atakayekuwa hakuridhika na matokeo itamlazimu kuziwasilisha kwa uongozi wa Tume ya Uchaguzi ili kuangaliwa ukweli wa matokeo hayo, lakini ikiwa mgombea huyo hakuwasilisha fomu hizo basi lalamiko lake halitosikilizwa”alisema Mzirai.

Akitoa mfano wa kauli hiyo Mzirai alisema kuwa katika Uchaguzi uliopita kuna mgombea mmoja wa nafasi ya urais alijitangaza kushinda na kulalamika hadi Tume ya Uchaguzi lakini Tume ilimtaka kuleta ushahidi wa fomu maalum ya matokeo ya kuonesha takwimu ya matokeo zinazotolewa katika vituo vya kupigia kura lakini mgombea huyo alishindwa kuwasilisha fomu hizo.

Alidokeza kwa kusema kuwa ili kuhakikisha kuwa mgombea huyo mmoja ambaye alijitokeza na kutangaza kuibiwa kura yeye analo gazeti ambalo liliweza kuchapisha taarifa hiyo.

 

Mzirai akichambua mada zilizowasilishwa katika mkutano huo alisema kuwa katika mada iliowasilishwa na Msajili Msaidizi kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama Vya Siasa Ibrahim Sapi Mkwawa, ilisema kuwa kila Chama kinapaswa kutoa elimu sahihi kwa wafuasi wake juu ya suala la siku ya upigaji kura.

Elimu hiyo ni vema ilenge zaidi kwa kuwafahamisha kuwa baada ya upigaji kura wanapaswa kurudi majumbani au kwenda katika shughuli zao za kijamii kama ilivyo kwa siku nyengine ili kuepusha kufanyika kwa vitendo viovu.

“Hatutopenda kuona mkusanyiko katika vituo vya upigaji kura hivyo ni vyema kwa kila atakaye maliza kupiga kura arudu nyumbani au aendelee na harakati zake za maisha kama kawaida”alinukuu Mzirai maneno ya Mkwawa aliyoyatoa wakati akiwasilisha mada katika mkutano huo.

Mwenyekiti huo amewataka wanasiasa kuongea na wafuasi wao watakapomaliza kupiga kura kurudi nyumbani kusikiliza matokeo kupitia vyombo vya habari na kujiepusha na vichocheo vya vurugu kama kukusanyika maeneo ya nje.

“Wanasiasa mwanasihi wafuasi wenu wakimaliza kupiga kura warudi nyumbani kuendelea na shughuli zao za kawaida kama unakwenda kuwaangalia wagonjwa nenda kama unaenda dukani endelea na shughuli zenu za kawaida” alisema.

Akiongeza kunukuu mada iliwasilishwa na Mkwawa Mzirai alisema kuwa kila mwananchi atapaswa kuangalia matokeo ya Uchaguzi kwa wagombea wote yatakayobandikwa katika vituo vyote vya Uchaguzi.

Alisema kuwa fursa hiyo kwa wananchi hao itapatikana mara baada ya watendaji wa Tume ya Uchaguzi kumaliza zoezi zima na upigaji kura ya kuhesabu pamoja na kupandika nakala katika vituo vya kyupigia kura.

“Kila mwananchi anapaswa kuona matokeo ya Uchaguzi lakini fursa hiyo itakuwa baada ya kubandikwa kwa fomu ya matokeo katika kila kituo, hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kuangalia, kupiga picha, kurusha kwenye wasap au kwa vyovyote vile atakavyoona inamanufaa kwa upande wake”alisema Mzirai.

Aidha Mzirai alisema kuwa kila Chama kina jukumu la kuchagua Mawakala watakao waamini katika kushughulikia harakati zote za upigaji kura na kuhesabu ili kuepusha lawama za kuibiwa au kufanyiwa mchezo mchafu.

Alisema kuwa Vyama vikifuata utaratibu huo utaweza kuwasaidia katika kuepukana na lawama hasa wakati wa matokeo yatakapotangwa katika vituo vya upigaji kura.

Kwa  upande wa uwekaji wa amani kwa kipindi chote cha uchaguzi Naibu Ispekta Jenerali wa Polisi DIGP Abdulrahman Kaniki, kutokaMakao Makuu ya Polisi wakati akiwasilisha mada katika mkutano huo alisema kuwa Jeshi la Polisi linatoa ulinzi kwa Vyama Vyote vya Siasa.

Kaniki alisema kuwa suala la ulinzi ambao unatolewa na Jeshi hilo ni kwa Vyama vyote tena bila ya hata upendeleo huku akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni jukumu la Jeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ya Uchaguzi.

“Jeshi la Polisi limeahidi kufanya kazi zake kwa weledi na busara na pale panapotokea hali inayoashiria uvunjifu wa amani siku au wakati wa Uchaguzi viongozi waVyama vya Siasa wasisite kutoa taarifa kwao mara moja”alinukuu Mzirai kauli ya Jeshi la Polisi iliyotelewa na Naibu Ispekta Jenerali wa Jeshi hilo.

Mzirai alisema kuwa kwa upande wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khamis Khamis wakati wakiwasilisha mada juu ya usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Uchaguzi wamevitaka Vyama Vya Siasa kuendelea kuzingatia maadili ya Uchaguzi kwa kuwa shauku ya kila mtanzania ni kuona Uchaguzi unamaliza kwa amani.

Mzirai alimalizia kwa kwa kuvitaka Vyama Vya Siasa kuachana na baadhi ya propaganda za baadhi ya Vyma akisisitiza kuwa Uchaguzi mara huu wanatarajia utakuwa huru na haki.

 

 

Advertisements

One Reply to “Piga kura rudi nyumbani – Mzirai”

  1. Mzirai alisema kuwa kwa upande wa Tume ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva ambaye ni Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) na mwakilishi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Khamis Khamis wakati wakiwasilisha mada juu ya usimamizi na utekelezaji wa maadili ya Uchaguzi wamevitaka Vyama Vya Siasa kuendelea kuzingatia maadili ya Uchaguzi kwa kuwa shauku ya kila mtanzania ni kuona Uchaguzi unamaliza kwa amani.===== (( Amma shauku ya kila Mtanzania ni kuona uchaguzi unafanyika kwa uadilifu na kwa haki …))
    ………

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s