Maalim Seif: Hakuna wa kuzuia mabadiliko Oktoba 25

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF chini ya mwamvuli wa Ukawa, Maalim Seif Sharif
Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF chini ya mwamvuli wa Ukawa, Maalim Seif Sharif

Zanzibar. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF chini ya mwamvuli wa Ukawa, Maalim Seif Sharif Hamad amesema hakuna wa kuyazuiya mabadiliko yajayo kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Maalim amekionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisijaribu kuleta vurugu kitakaposhindwa katika uchaguzi huo akisema Tanzania ni nchi ya amani hivyo chama hicho tawala lazima kikubali kushindwa ikibidi.

Akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni katika Viwanja vya Shule ya Mkwajuni, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja, Maalim Seif amesema CUF kitashika madaraka kwa kutegemea nguvu za Mwenyezi Mungu na hayuko wa kuzuia hivyo CCM isijidanganye kwa kuandaa hujuma za aina yeyote.

“Nawasihi sana vijana msikubali kuchokozeka hawa jamaa wanajaribu kupanga kila mbinu kukuchokozeni wameishiwa msikubali kuingia katika vurugu. CCM lengo lao ni kuchokoza ili kusitisha uchaguzi’, amesema Maalim.

Maalim Seif amewaambia vijana wasijaribu hata kidogo kumtukana wala kumkejeli Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akisema ni wakati wa kusubiri mabadiliko kwa kipindi cha siku 10 zijazo, ambapo CUF wanaelekea kushika madaraka ya kuongoza nchi.

Maalim Seif ametoa angalizo kwa Tume za Uchaguzi kuzingatia uadilifu na kuharakisha upatikanaji wa matokeo ili kuepusha mazingira yeyote ya ubadhirifu.

Tamko lililolipua shangwe katika mkutano huo ni pale Maalim alipotangaza kupitia mkutano huo kwamba Jumamosi hii ni siku rasmi ya kutangaza na kuzindua mkakati wake wa kuigeuza Zanzibar kuwa Singapore ya Afrika.

Maalim Seif ameyasema hayo akieleza kwamba ni sehemu ya lengo la ziara yake Nchini Afrika ya Kusini, alikotembelea na kukutana na wadau mbali mbali wa uchumi walioahidi kusaidia utekelezaji wa azma hiyo, kuanzia Jumatatu ya wiki hii.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s