Ahongwa gari, fedha kupambana na Balozi Seif

Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu Mhe Haji Omar Kheri akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein, katika viwanja vya bumbwini makomba na kumuombea Kura Dk Shein, ili kuendeleza amani na utilivu na Masendeleo ya Wazanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Tumbatu, Haji Omar Kheri akiwahutubia Wananchi katika mkutano wa kampeni ya Mgombea wa CCM Dk Shein, katika viwanja vya bumbwini Makomba na kumuombea kura Dk Shein.

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), katika Jimbo la Mahonda, wametahadharishwa juu ya kuwapo kwa njama za makusudi zinazoandaliwa na Chama cha Upinzani za kuhakikisha wanamnyima kura Mgombea wa Uwakilishi katika Jimbo hilo, Balozi Seif Ali Iddi.

Kauli hiyo ilitolewa na Faraji Ramadhani Faraji, ambaye alikuwa mgombea wa nafasi ya Uwakilishi, katika kura za maoni katika Jimbo la Mahonda, ambapo alichuana na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi.

Kwenye kinyang’anyiro hicho, Faraji alipata kura 441, huku Balozi Seif Ali Iddi, alifanikiwa kushinda katika Jimbo hilo, kwa kupata kura 1,638 na kumshinda mgombea huyo.

Akitoa maelezo yake mbele ya Wanachama wa CCM, walioshiriki mkutano wa shukrani, uliowahusisha wagombea walioteuliwa na Chama hicho kuwania nafasi ya Ubunge, Uwakilishi na Udiwani, mwanachama huyo alisema kuna hujuma zimeandaliwa kumuangusha mgombea wa Uwakilishi katika Jimbo hilo.

Mwanachama huyo alisema, baada ya kumalizika kwa kura ya maoni alifuatwa na moja ya chama cha Upinzani na kumtaka kuwania nafasi ya Uwakilishi kwa Jimbo hilo kupitia chama hicho kwa vile wako tayari kumpa gari na fedha, ili aweze kushindana na Mteule huyo wa CCM.

Alisema viongozi hao walimueleza kuwa sababu kuu ya kumchukua yeye kwa vile tayari wamebaini ana uwezo wa kuungwa mkono kupitia vijana aliowatumia kufanya kampeni zake wakati wa kura za maoni.

Fadhil, alisema katika kutakiwa kufanikisha hilo, aliwahi kuitwa mara mbili katika vikao vya Mkakati na chama hicho, ambavyo vilifanyika Mjini, jambo ambalo alilikataa kulitimiza hilo na kueleza kuwa ataendelea kubakia akiwa katika CCM.

Kutokana na hali hiyo, Fadhil, alieleza kuwa ni vyema wananchi wa Jimbo hilo, wakaziona njama hizo, kwa vile tayari hivi sasa baadhi ya viongozi hao waliwafuata vijana waliomuunga mkono katika kura za maoni na kuwataka kuingia katika upinzani.

Fadhil, alisema tayari vijana hao walimfuata kwa ushauri, lakini aliwataka kuwaepuka kwa vile yeye bado dhamira yake kuendelea kuwemo ndani ya CCM na sio vyama vya Upinzani.

Mwanachama huyo, aliwataka wanachama wenzake, kuiona hatari hiyo, na kuiepuka kwa vile inaonesha ni jambo lililoandaliwa kwa makusudi kumuangusha Balozi Seif katika uchaguzi huo.

Akizungumza katika kikao hicho, Balozi Seif, alisema anatambua kuwepo kwa ukweli huo, kutokana na baadhi ya wagombea wa upinzani, wamekuwa wakiyachukua makundi ya vijana na kuwalaghai kwa ahadi mbalimbali ili waachane na dhamira zao za kukipa ushindi Chama hicho.

“Sijui nilichowafanya, nimejaribu kufuatilia hili, nimeona huu ni mpango unaoandaliwa kwa makusudi lazima mimi nishindwe, lakini hilo halitafikia nitahakikisha nitashinda katika uchaguzi unaokuja na wanachama wa CCM nipeni kura zenu”, alisema Balozi Seif, ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais.

Alisema tayari hivi sasa, ameshajiandaa kufanya mabadiliko mbalimbali ya shughuli za kimaendeleo, ikiwemo kufikisha huduma ya umeme katika kijiji cha Kichungwani, baada ya kumalizika kwa kazi ya kusambaza umeme kijiji cha Matetema.

Eneo, jengine ambalo alilitaja ni kuona wanawapatia huduma ya maji kwa vijiji ambavyo bado hawana huduma hiyo, pamoja na kustawisha ustawi wa skuli za Jimbo hilo, ambazo bado hazina vikalio.

Aidha, Balozi Seif, aliwaahidi makundi ya Wanawake na vijana, kuwapatia mitaji itayoweza kuwasaidia kuwa na njia za kukabiliana na maisha yao.

Nae Mgombea Ubunge katika Jimbo hilo, Bahati Ali Abeid, alisema Wanawake na vijana hawatajuta kuwachagua wagombea kutoka CCM, kwani tayari anakusudia kuwawezesha ili waweze kufanya kazi za uzalishaji mali katika sekta ya kilimo kwa kuwaanzishia kilimo cha mboga mboga.

Chanzo: Zanzibar Leo

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s