Watanzania wanne wapoteza maisha kwa mkanyagano Makka

Picha+MakkaDar es Salaam. Watanzania wanne ni miongoni mwa mahujaji zaidi ya 700 waliopoteza maisha jana kwa mkanyagano wakati wakitekeleza ibada ya hija mjini Mina umbali wa takribani kilometa tano toka mji mtakatifu wa Kiislamu, Makka nchini Saudi, Arabia.

Taarifa iliyotolewa na Baraza Kuu la Kiislamu nchini (Bakwata) na kuthibitishwa na Katibu Mkuu wake, Suleiman Lolila imewataja waliopoteza maisha kuwa ni Mwanaisha Hassan Juma, Mkongwe Suleiman Hemed na Seif Said Kitimla.

Hadi jana usiku taarifa hiyo iliyosainiwa na Sheikh Mkuu, Abubakari Zubeir bin Ally imesema jina la marehemu mmoja ambaye anafanya idadi ya mahujaji waliofariki kufikia wanne bado halijapatikana.

Taarifa hiyo inasema, mahujaji wengine wawili wanawake wa Tanzania haijulikani walipo na kwamba baraza hilo limeshindwa kuwa na uhakika na hali zao za kiafya iwapo wako hai ama wamekufa.

Katika taarifa hiyo, Mufti Zubeir amesema mwanamke mmoja raia wa Kenya aliyefahamika kwa jina la Fatuma Mohamed Jama amekufa katika ajali hiyo mbaya kuwakumba mahujaji katika siku za karibuni na kwamba mwanamke huyo alisafiri kwa kutumia mawakala wa Kitanzania.

Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia umeliambia Mwananchi Digital kuwa upo uwezekano idadi ya vifo ikaongezeka baada ya makampuni kadhaa yanaosafirisha mahujaji kwenda hija kuripoti kupotelewa na wateja wao.

“Idadi inaweza kuongezeka kwa kuwa makampuni kadhaa yameripoti kupotelewa na wateja wao. Hivi sasa tunafuatilia taarifa hiyo na kwamba tutaujulisha umma wa watanzania baada ya zoezi hilo kukamilika” amesema Kaimu Balozi, Ahmada Sufiani.

Mkanyagano wa mahujaji ulitokea jana mjini Mina, yapata kilometa tano toka mji Mtakatifu wa Kiislamu, Makka na kusababisha vifo vya mahujaji zaidi ya 700 na kujeruhi wengine zaidi ya 850.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s