Ni Gwaride la mwisho kwa awamu hii

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya Gwaride la KIKOSI cha Polisi FFU mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo (kushoto)Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame.
Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein akipokea salamu ya heshma ya Gwaride la Kikosi cha Polisi FFU mara alipowasili katika viwanja vya Chuo cha Amali Mkokotoni katika Mkutano wa Baraza la Eid El Hajj akiwa mgeni rasmi katika baraza hilo leo (kushoto)Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Moammed Shein hii ni mara yake ya mwisho kupokea Gwaride katika kipindi hiki cha uongozi wake wa miaka mitano , Dk Shein ameingia katika kinyanganyiro cha kuwania na kutetea nafasi yake hiyo huku akipata upinzani mkali kutoka kwa mpinzani wake kutoka Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad ambaye yeye atakuwa ni mara ya nne anawania nafasi hiyo ya uongozi.

Dk Shein ni mara yake ya pili tokea kuteuliwa na Chama Chake Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo ya urais wa Zanzibar ambayo hushikiliwa kwa muda wa miaka mitano kwa mujibu wa sheria na katiba ya Zanzibar inavyoelekeza.

Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) akijumuika na Viongozi mbali mbali na Waislamu  katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A,palipofanyika Swala ya Eid El Hajj iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi

Akihitubia katika mkutano wa Baraza la Eid El Hajj huko katika Chuo Cha Mafunzo ya  Amali Zanzibar Mkokotoni Mkoa wa Kaskazini aliwataka viongozi wa kisiasa na wa kidini kuhubiri amani na mshikamano katika kipindi hichi cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu.

Viongozi mbali mbali na Waislamu  wakiwa katika Swala ya  Eid El Hajj katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A, iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi

Shein ameyasema hayo jana wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja kwenye Baraza la Idi lililofanyika kwenye Ukumbi wa kituo Cha Mafunzo ya Amali-Mkokotoni, nje kidogo ya mji wa Unguja.

Akina mama wa Kijiji cha Mkokotoni na Vijiji Jirani walijumuika katika Swala ya  Eid El Hajj katika Uwanja vya Mpira Mkokotoni Wilaya ya kaskazini A, iliyoswaliwa kitaifa katika Mkoa wa Kaskazini Unguja leo iliyoongozwa na Sheikh Mmadi Shamata Kutoka Msikiti wa Kijiji cha Nungwi

Dk Shein amesema amani ni jambo muhimu sana kwa nchi yoyote duniani, kwani bila ya amani hawataweza kupata maendeleo ,na hivyo kunaweza kukahatarisha uhai wa watu na kuharibu miundombinu mbali mbali na kuzua fadhaa katika jamii yetu.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na Makamo wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, wakati akishiriki sala na baraza la Eid El-Hajj Mkokotoni.

“Napenda kuwakumbusha na kuwasisitiza viongozi wa kisiasa na wa madhehebu ya dini kusisitiza wafuasi wetu umuhimu wa kulinda amani na kujiepusha na vietendo vyovyote vile vinavyoweza kutuondolea amni na utulivu tulionao” Alisema Dr Shein.

Rais Shein ambaye pia ni mgombea wa urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, aliahidi kwamba Serikali yake itakabiliana vikali na wale wote watakaojihusisha na vitendo vitakavyoashiria uvunjifu wa amani.

Pamoja na hayo Dr, Shein alitumia hotuba yake kuelezea mafanikio yaliyofikiwa na Serikali yake kwa wananchi wa Mkoa huo kuwa ni pamoja na kuimarisha upatikanaji wa maji safi na salama ambapo amesema hali ya upatikanaji wa maji hayo umefikia asilimia 71.68.

Katika sekta ya Afya, Shein amesema ameimarisha hospital ya Kivunge na vituo vyengine vinayopatikana kwenye mkoa huo kwa lengo la kuwahudumia wananchi.

Hata hivyo ametoa wito kwa wanachi wa Mkoa huo na Zanzibar kwa ujumla kuhakikisha wanawapeleka watoto wao kwenye kituo cha mafunzo ya ufundi cha Mkokotoni kwa lengo la kujiendeleza.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s