Shein aahidi kudumisha mapinduzi-

pic+sheinChama cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar leo wamezindua rasmi kampeni za kitaifa kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka huu. Shughuli hizo za uzinduzi zimefanyika kwenye Uwanja wa Kibandamaiti visiwani humo na CCM Zanzibar wazindua rasmi kampeni,  kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa chama hicho akiwemo Rais Jakaya Kikwete, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

Kwa awamu nyingine, Dk Ali Mohamed Shein amepewa ridhaa ya kupeperusha bendera ya CCM kwa ngazi ya urais akipambana na wagombea wengine wa upinzania akiwemo Maalim Seif Sharif Hamad wa CUF anayeungwa mkono na Ukawa.

Dk Shein amesema ataendelea kuyalinda, kuyatetea na kuyaendeleza mapinduzi ya Zanzibar kwa manufaa ya watu wake. Pia amesisitiza kuwa umoja, amani na utulivu ndiyo nguzo ya maendeleo ya taifa lolote duniani, hivyo serikali yake itahakikisha Zanzibar inaendelea kuwa na umoja, amani na utulivu.

Kama ilivyo kwa bara, wazungumzaji takriban wote waliopewa nafasi ya kuzungumza walitumia muda mwingi kuuzungumzia upinzani hususani wagombea wa Ukawa akiwemo Maalim Seif na Juma Duni Haji.

Rais Jakaya Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa, amemkabidhi Dk Shein Ilani na Katiba ya chama hicho kama nyenzo muhimu anazopaswa kuzitumia wakati wote wa kampeni ili kujipatia ushindi Oktoba 25.

Mkutano huo kama ilivyo mikutano mingine ya kisiasa, umehudhuriwa na idadi kubwa ya wananchi waliofika kusikiliza sera za CCM.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s