Wawili wafa kwenye mkanyagano mkutano wa Magufuli Morogoro

Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro
Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli akihutubia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro

Watu wawili wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na mkanyagano uliotokea jana Uwanja wa Jamhuri, Morogoro katika mkutano wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Tayari leo(jana), Mwenyekiti wa CCM taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amewatembelea majeruhi hao waliolazwa Hospitali ya Mkoa Morogoro.

Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Dk Ritha Lyamuya amesema walipokea watu 19 waliokuwa na majeraha yakiwemo ya kuvunjika maeneo mbalimbali ya mwili na kuongeza kuwa miongoni mwao, wawili walikufa kutokana na kuumia vibaya.

Aidha Dk Lyamuya alisema kuwa wagonjwa ambao bado wamelazwa wako 10 na wengine saba walitibiwa na kuruhusiwa.

Dk Lyamuya alisema kuwa waliokufa ni pamoja na mwanamke anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 42 na mtoto wa umri wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhan Abdalah.

Uwanja wa Jamhuri jana ulifurika watu wakati mgombea urais kwa tiketi ya CCM John Magufuli alipokwenda kwa ajili ya kufanya kampeni.

Mara tu baada ya Magufuli na viongozi wengine kuondoka uwanjani hapo, ndipo hali ya kusukumana na kukanyagana ilitokea getini wakati watu wakitoka.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s