Dk. Shein, Maalim Seif kimeeleweka urais Z’bar

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Jecha Salim Jecha

Mgombea urais wa Zanzibar kupitia United Democratic Party (UPDP) Mwajuma Ali Khamis, ameshindwa kurejesha fomu na kukosa sifa ya kugombea.

Mwajuma alikuwa miongoni mwa wagombea  15 waliochukua fomu Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (Zec).
Tume hiyo jana jioni ilifunga urejeshaji wa fomu na kuwataja wagombea ambao walitimiza masharti.
Akizungumza na waandishi wa habari, baada ya urejeshaji fomu kufungwa, Mkurugenzi wa Zec,  Salum Kassim Ali, alisema wagombea 14 wametimiza masharti na wanasubiri pingamizi kutoka kwa mtu yeyote wakiwamo wagombea wa nafasi hiyo.
“Kama kuna mgombea mwenye pingamizi dhidi ya mgombea mwenzake ajitokeze ndani ya saa 24 kabla ya kuanza kwa kampeni,” alisema.
Alisema Zec imeridhika na vielelezo walivyowasilisha na wagombea hao.
Alisema kuanzia leo wagombea na vyama wana haki ya kuanza kampeni na kusisitiza kuwa ni lazima kufuata maadili ya uchaguzi.
Mgombea  wa NRA, Seif Ali Iddi, alifika ofisi za Zec muda mfupi kabla ya kufungwa urejeshaji wa fomu.
Alifika saa 9: 52 zikiwa ni dakika nane kabla ya saa 10:00 jioni.
Mgombea alieleza kuwa alichelewa kutoka na  alipata ajali ya kugongwa na gari eneo la Maisara.
Wagombea waliopitishwa na Zec ni Dk. Ali Mohammed Shein (CCM); Maalim Seif Sharif Hamad (Cuf); Hamad Rashid Mohamed (ADC); Khamis Iddi Lila (ACT – Wazalendo); Seif Ali Iddi (NRA); Juma Ali Khatib (Tadea); Ali Khatib Ali (CCK); Abdallah Kombo Khamis (DP) na Kassim Bakari Ali (Jahazi Asilia).
Wengine ni Issa Mohammed Zonga (Sau); Tabu Mussa Juma (DM); Haafidh Suleiman (TLP); Said Soud (AFP) na Mohammed Masoud Rashid (Chaumma).
Ikiwa hapatakuwapo na pingamizi, wagombea wawili ambao watachuana vikali kutokana na vyama vyao kuwa na wafuasi wengi ni Rais Shein na Maalim Seif.
Chanzo: Nipashe
Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s