Rose Kamili, Askofu Kilaini wamshukia Dk Slaa

Mbunge wa viti maalumu wa Chadema, Rose Kamili akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana kuhusu kauli aliyoitoa aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa . Kushoto ni binti wa Dk Slaa, Emiliana Slaa na Linus Slaa. Picha: Mwananchi
Mbunge wa viti maalumu wa Chadema, Rose Kamili akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana kuhusu kauli aliyoitoa aliyekuwa katibu mkuu wa Chadema, Dk Willibrod
Slaa . Kushoto ni binti wa Dk Slaa, Emiliana Slaa na Linus Slaa. Picha: Mwananchi

Dar es Salaam. Kauli ya Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema Dk Willibrod Slaa kuhusu
hatma yake kisiasa imeendelea kutikisa baada ya mke wake wa zamani, Rose Kamili kuibuka na kusema amesikitishwa na kauli alizozitoa mume wake huyo alipozungumza na waandishi wa habari Septemba Mosi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kamili alisema wakati Dk Slaa anatangaza kung’atuka kwenye siasa alisema amekuwa akila mihogo na familia yake, jambo ambalo si la kweli.

Alisisitiza kuwa japokuwa mihogo siyo chakula kibaya lakini watoto wake, Elimiana na Linus Slaa hawakuwahi kuishi kwa kutegemea chakula hicho ingawa walitelekezwa na baba yao tangu mwaka 2010.

Kamili ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa wa Chadema, alisema Dk Slaa aliwadanganya
wananchi aliposema kuwa haongei na mgombea wa urais wa Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa na Waziri Mkuu wa zamani Frederick Sumaye kuwa siyo kweli kwa kuwa amekuwa akiwasiliana na viongozi hao.

Alisimulia kuwa mwaka 1995 wakati Dk Slaa alipoenguliwa na CCM kugombea ubunge Jimbo la Karatu, alikwenda nyumbani kwa Lowassa kuomba ushauri.

“Lowassa alisema ‘mimi nakushauri ujiunge na chama chochote’” alisema Kamili na kuongeza kuwa marafiki zake Dk Slaa nao walimshauri aingie chama chochote.

“Mimi namshangaa anavyosema haongei na Lowassa… hizo chuki anazosema yeye kama padri mstaafu zinatoka wapi?,” alisema Kamili.

Kuhusu Sumaye, Kamili alisema kuwa wiki tatu zilizopita alipigiwa simu na kiongozi huyo
akimuulizia namba ya Dk Slaa, baada ya kumtafuta kwenye simu yake bila mafanikio.
“Aliniuliza mbona simu yake haipatikani, nikampa akampigia wakaongea,” alisema.

Mjini Bukoba, Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Methodius Kilaini amesema
anamshangaa Dk Slaa kutoa tuhuma dhidi ya maaskofu kwa kuwa aliwahi kuwa Katibu wa
Baraza la Maskofu na anajua wanavyofanya kazi.

Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi mjini Bukoba, Askofu Kilaini alisema Maaskofu hawanunuliki na kanisa halifungamani na upande wowote wa kisiasa huku akidai huenda kauli hiyo ilimponyoka.

Kauli ya Askofu Kilaini imetolewa ikiwa ni baada ya siku chache zilizopita aliyekuwa Katibu
Mkuu wa Chadema, Slaa kutangaza kustaafu siasa huku akiwatuhumu baadhi ya maaskofu kupokea rushwa kutoka kwa mmoja wa wagombea.

‘’Wanasiasa ni wachangiaji wazuri katika hafla mbalimbali za kanisa lakini hata siku moja
huwezi kusema maaskofu wamenunuliwa Kanisa linashikilia maadili na kuombea amani kwa Taifa,’’ alisema Kilaini

Pia Askofu Kilaini aliongeza kuwa matamko kama yaliyotolewa na Dk Slaa yanaweza
kusababisha mkanganyiko kwenye jamii, huku akionya hatari ya dini kutumika kwenye
mijadala kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Aidha alirejea mwaka 2000 kuwa baada ya vurugu kuanza kutokea Zanzibar na wananchi
kukimbia, waliitana viongozi wa madhehebu yote ya dini na kutoa tamko la pamoja wakionya dini zisihusishwe kwenye harakati za kisiasa.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s