Maalim Seif arejesha fomu za Urais wa Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akikabidhi fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar

Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, leo amerejesha fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).

Maalim Seif amerejesha fomu hizo majira ya saa nne asubuhi katika ofisi za tume hiyo zilizoko Hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar, baada ya kukamilisha masharti yaliyowekwa na Tume hiyo.

Miongoni mwa masharti hayo ni pamoja na kula kiapo mahakamani pamoja kuambatanisha shilingi milioni mbili, mambo ambayo ametayatekeleza.

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Bw. Jesha Salim Jecha akionesha fomu za kugombea Urais wa Zanzibar, baada ya kukabidhiwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, huko hoteli ya Bwawani mjini Zanzibar

Baada ya kukabidhi fomu hizo kwa Mwenyekiti wa Tume hiyo Bw. Jecha Salim Jecha, Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, ameitaka tume hizo kufanya kazi kwa uhuru na uadilifu.

Amesema kufanya hivyo kutapelekea kufanyika kwa uchaguzi wa amani, huru na wa haki, jambo ambalo litailetea sifa kubwa Zanzibar katika jamii ya kimataifa.

Katika hafla hiyo, Maalim Seif ameambatana na baadhi ya viongozi wa Chama hicho wakiwemo Mgombea uwakilishi wa Jimbo la Malindi Mhe. Ismail Jussa Ladhu, Mgombea uwakilishi wa Jimbo  la Chukwani Mhe. Mansoor Yussuf Himid na Mratibu wa uchaguzi wa CUF Bw. Muhene Rashid.

Chanzo: OMKR

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s