Polisi yamtahadharisha Lowassa staili ya kampeni zake

Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa akishuka kwenye moja ya daladala
Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa akishuka kwenye moja ya daladala

Dar es Salaam. Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtahadharisha mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa kuwa kampeni alizoanza kwa kuyatembelea makundi kadhaa zinaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.

Hata hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia jeshi hilo kukabiliana na vitendo viovu.

Onyo hilo limetolewa ikiwa ni siku ya pili tangu Lowassa na mgombea mwenza Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi huku wakitumia usafiri wa umma.

Kwa kutumia staili hiyo, leo Lowassa akiwa na Duni Haji wametembelea maeneo ya Tandika, Tandale na Kariakoo jijini Dar.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova amesema ziara iliyofanywa leo maeneo ya Swahili, Kariakoo zimesababisha mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha shughuli za maendeleo.

Baada ya CCM kuzindua kampeni zake mwishoni mwa juma lililopita viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Chadema nacho kinajiandaa kufanya hivyo Agosti 29 maeneo hayohayo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

One Reply to “Polisi yamtahadharisha Lowassa staili ya kampeni zake”

  1. Tamko hilo la TAHADHARI la Polisi linaweza kutafsirika ktk maana mbili :-
    1- Ni kuonesha wasiwasi walionao chama tawala kwamba huenda mbinu aina hiyo inayotumika na UKAWA inaweza kuwavutia wananchi wengi na hatimaye mvuto huo ukaleta mabadiliko makubwa ktk uchaguzi mkuu ujao .
    2- Huenda kukawepo mikakati ya chini kwa chini itakayoandaliwa na chama tawala ktk kumdhuru MPINZANI huyo halafu wakatumia evidence hiyo kwamba serikali iliwahi kumtahadharisha Mgombea huyo na ndiyo yakamfika yaliomfika kwa kuendlea kufanya kampeni zake za aina hiyo..( wakati ambapo tayari limeshaandaliwa kundi maalum na hao hao kwa lengo la kumdhuru na kummaliza ) ..

    HAYA NI MAONI YANGU TU.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s