Sifichi… nayaje tupumue

Baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA, wakijitambulisha kwa wananchi wa Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti
Baadhi ya viongozi wakuu wa UKAWA, wakijitambulisha kwa wananchi wa Zanzibar kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Kibandamaiti

WAKUU wa dola hawana raha. Wala hawatulii – wawe vitini maofisini mwao au makochini wawapo majumbani. Ni hamkani nguo kichwani.

Waulize wamekumbwa na zahma gani hata wasumbuke au kuhangaika namna hiyo? Ukipewa jibu nchinje. Hupewi jibu bana, na yeyote kati yao.

Sanasana badala ya kupewa jibu la swali lako ambalo kusema kweli ni rahisi tu, watakusukumia kejeli na maskhara. Utasikia “makapi matupu.”

Wamesikilikana wakisema “wanakula matapishi.” Wengine ambao ni mabingwa wa kutema moto, wamesema “Hakuna lolote, ushindi wa tsunami utawashukia.”

Waungwana wa Ukawa si mnasikia waziwazi umoja wenu unaowakusanya na kutarajia mabadiliko yanayogusa matumaini yenu wanavouita Ukiwa, ndivyo walivyo, kila lenu jema wao kulikorofisha. Wakorofi wa enzi!

Labda nyie hamkusikia akisema, mimi nilimsikia mkuu wa kaya yetu ya Ukwamani iliyoboreshwa akisema bila soni wanao uwezo, wanayo na maarifa na wanaye mgombea bora kuliko wote ardhini petu.

Na-aape hajafuta matamshi yake ya kusimamia Sisiem kupata ushindi ama faima. Hajafuta. Hajatoa ufafanuzi eti alikosea. Wala hakuwa na sababu hata moja ya kurudia alichosema; mtu mwenyewe hajapata kukosea maishani. Kila jambo alifanya ndivo. Fundi mkubwa yeye.

Wanachama na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA, walivyojumuika kwenye mkutano huo uliofanyika Kibandamaiti
Wanachama na wapenzi wa vyama vinavyounda UKAWA, walivyojumuika kwenye mkutano huo uliofanyika Kibandamaiti

Huamini mwenzangu ufundi wake? Huyu hakiyamungu fundi, tena si fundi mchundo ivo. Fundi hasa wa mambo na vijimambo. Na-aape ninayemjua hakosei ndo maana anaendelea kufyatua na kufyatuka kusema amelewa asali.

Lakini tuwache haya mepesi yasomana. Yamepata lini maana wakati wao weshajipangia kushinda kwa tsunami na kiongozi amewahakikishia ni mabingwa wa maarifa ya ushindi wa namna hiyo?

Tatizo la Watanzania wa Tanganyika wamechelewa kuwaelewa Sisiem, tofauti na wenzao Wazanzibari. Kule usiseme kitu kuhusu wanaume hawa. Si kwa ufedhuli wa kisiasa wala ukakamavu wa uchafuzi wa uchaguzi, wajuzi wa haja.

Huanza mbali usivyotarajia. Wenyewe kweli wanaamini hasa uchaguzi huanza mara baada ya uchaguzi. Sasa nyie wenzangu na mie mnasubiri miaka miwili kabla ya siku ya kuvoti ndo mnajipanga. Hapo wao tayari hisabu zimekamilika. Wanakamilisha hisabu mapema kwa kujua biashara asubuhi jioni hisabu.

Mlisikia hapa karibuni mazombi – walewale washenzi waliojigeuza kutoka Janjaweed wakibeba bunduki za sirikali na kusindikizwa na polisi wa jenerali Maangu – walishambulia wananchi wema? Kumbe mlidhani maskhara, walikuwa wamo katika kutumikia mabwana zao waliotaka hisabu ikamilishwe kabla jua kuchomoza.

Baadhi ya wananchi jamii ya kimasai waliopo Zanzibar, walivyojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa UKAWA kumuunga mkono mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Mhe. Edward Lowassa
Baadhi ya wananchi jamii ya kimasai waliopo Zanzibar, walivyojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa UKAWA kumuunga mkono mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA Mhe. Edward Lowassa

Nilisema hapa mimi nanyi tunapobwaga nyoyo zetu, daftari linapita; tena kote majimboni laakin, msishangae mkakuta limepita na wengi wenu mkikosa kuandikwa. Kama kila mtu ame, jambo la kufurahia.

Napenda mnavyoziita kadi zenu “kichinjio.” Sawawa, hakuna isipokuwa kuzitumia kumchinja adui ifikapo 25 Oktoba. Sote tukichinja, nyama tutakula sote. Ole wako usije kuchinja, umetukosesha nyama tamu.

Ila si busara kuondoka nisiseme Ewe Mola Muumba, walinde viongozi wa UKAWA watimize matarajio ya watu wa jamhuri hii inayotafunwa kama shamba la bibi. Nifiche lipi kuwa mi mtaka mabadiliko? Sifichi ng’o, na yaje tupumue!

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s