Kamati ya uchaguzi CCM hadharani

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye
Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, (Itikadi na Uenezi), Nape Nnauye

Dar es Salaam. Chama cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kamati ya wajumbe 32 mahususi kwa ajili ya kempeni za Uchaguzi Mkuu 2015 chini ya Mwnyekiti Abdulrahman Kinana. Akizungumza na wanahabari katika Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumumba, jijini
Dar es Salaam leo, Katibu wa Uenezi wa CCM amesema Kinana atasaidia jukumu
hilo na makamu wenyeviti wawili; Rajabu Luhavi (Bara), Vuai Ali Vuai (Z’bar).

Mbali na viongozi hao, kamati inaundwa na wajumbe wengine kutoka Tanzania Bara na
Visiwani wakiwemo makada Sophia Simba, Asha-Rose Migiro, Mwigulu Nchemba na Nape Nnauye.

Wengine ni January Makamba, Stephen Wassira, Shamsi Vuai Nahodha, Lazaro Nyalandu, Bernard Membe, Ummy Mwalimu Pamoja na Makongoro Nyerere.
Wanakamati wengine ni Maua Daftari, Mahmoud Thabiti Kombo, Christopher Ole Sendeka, Harrison Mwakyembe, Stephen Masele, Shaka Shaka na Pindi Chana.

Wakati huohuo, Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi amesema Kamati Kuu ya CCM imewaidhinisha Jonathan Njau kuwa mgombea ubunge jimbo la Singida Mashariki pamoja Emmanuel John atakayepeperusha bendera ya CCM jimbo la Kiteto.

Uchaguzi wa awali katika majimbo hayo ulilazimika kurudiwa baada ya chama hicho kutangaza kuwa kulikuwa taratibu zilivunjwa. Majimbo mengine ambayo CCM ililazimika kurudia kura za maoni ili kuwapata wagombea ubunge ni Rufiji, Busega, Makete, Ukonga na Kilolo.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s