Profesa Lipumba: CCM ina wagombea wawili wa urais

lipumbaDar es Salaam. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), kina wagombea wawili wanaowania kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Madai hayo mapya ya Profesa Lipumba yametolewa siku tatu baada ya kujiuzulu uenyekiti CUF, akisema hiyo ni moja ya sababu za kuachia nafasi yake kutokana na uamuzi uliofikiwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kuhusu mgombea urais.

Akizungumza wakati akitangaza kujiuzulu wiki iliyopita, Profesa Lipumba alisema dhamira yake ilikuwa inamsuta kwa kuwaingiza ndani ya Ukawa watu kutoka CCM, waliokuwa wanapingana na maoni ya wananchi kuhusu rasimu ya Katiba ya Jaji Warioba na kuwapa fursa ya kuwania urais.

Juzi usiku katika mahojiano aliyoyafanya na Azam TV kutoka Kigali alikosema anafanya utafiti, Profesa Lipumba alisema kumpa nafasi waziri mkuu mstaafu, Edward Lowassa kuwania urais kupitia Chadema ndani ya Ukawa, ni sawa na CCM kusimamisha wagombea wawili (Lowassa) na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli.

Katika mahojiano hayo ya simu, Profesa Lipumba ambaye wiki mbili zilizopita alimpokea Lowassa akisema ni mtu safi na kwamba, ufisadi ndani ya CCM ni mfumo  alisema katika kujiuzulu kwake hakutumiwa na CCM kuparaganyisha Ukawa, bali walikuwa tayari wameparaganyika.

“Ukweli ni kwamba tumejiparaganyisha wenyewe ndani ya Ukawa. Kwa hiyo Watanzania watakuwa na wanaCCM wawili wanaogombea urais wakati Ukawa tulikuwa na wagombea watatu… mimi, Dk Willibrod Slaa, (Katibu Mkuu wa Chadema) pamoja na Dk George Kahangwa (NCCR-Mageuzi) ambaye alikiri kuwapo makubaliano hayo.

“Tulikutana nyumbani kwangu tukakubaliana Dk Slaa apeperushe bendera ya Ukawa, lakini tumewekwa kando,” alisema Profesa Lipumba.

Alisema yupo Rwanda kwa muda na anafanya utafiti kuona namna gani Tanzania inaweza kujifunza mambo ya kiuchumi kutokana na nchi hiyo kupiga hatua kubwa kiuchumi.

Pia alisisitiza kuwa hajahama nchi na kwamba wiki hii anatarajia kurejea nchini.

Agosti 6, mwaka huu Profesa Lipumba alijivua  uenyekiti wa CUF wakati mkakati wa vyama vya upinzani kushirikiana kushika dola ukiwa umeshika kasi.

Advertisements

One Reply to “Profesa Lipumba: CCM ina wagombea wawili wa urais”

  1. Maneno ya Prof. Lipumba yanahitaji kuzingatiwa sana na kuyatafakari kwa undani kabisa. Watanzania kwa asilimia kubwa kbs ni watu waliozoeshwa kudanganywa na vyombo vya habari , bila ya kuzifanyia tathmini HABARI zenyewe na bila ya kuzifanyia utafiti ….wamekuwa kama wamerekani kule kwao ambapo vyombo vya habari ( media ) karibuni vyote vinamilikiwa na kuendeshwa na wale mamerekani wenyewe asili ya kiyahudi ambao huitwa Zionists. Na huku kwetu Africa pamoja na nchi yetu hii ya Tanzania -wapo wanaovihudumiya na kuvimiliki na kuviendesha vyombo vya habari kwa lengo tu la kujinufaisha aidha Taasisis zao au vikundi vyao ikiwa ni vya kisiasa au vya kidini – Na magazeti hayo yanazidi kuongezeka nchini Tanzania.
    Watanzania wanatakiwa wafanye tathmini na utafiti ktk kila jambo wanalolisikia –na utafiti mzuri wa wana falsafa ni ule Mtu anapotulia na kujiuliza masuali A to H ….na sio kulupuka tu na kufanya maamuzi ya haraka au kufata upepo unapoelekea -….Watanzania wengi bado kbs hawajaelimika na pia hawakomaa kisiasa kwa hiyo ni rahisi kwao kutegwa na kunaswa na kujikuta wakishidnwa kujitoa ktk mnasa -kwani wajanja hutumia mbinu tofauti ktk kufanikisha malengo yao……Na ndio maana mtu msomi kama mwnzetu Prof. Lipumba bila shaka ameyafanyia uchunguzi na utafiti hali ya kisiasa nchini na kutathmini hali ilivyo hivi sasa —Huenda yule adui yako akaingia nyumbani kwako kwa kuvaa vazi jengine na kujibadilisha –ili usimtambue …hatimaye anapofika ndani na kujua siri za humo na udhaifu uliopo au ukubwa uliojificha basi adui huyo huyo ni rahisi kwake kusambaratisha familiya yako au kupata mwanya wa kufanya madhara akiwa humo humo ndani bila ya wewe kujua : kwa kauli yake hiyo Prof.LIPUMBA ilikuwa ni kuwapa watanzania TAHADHARI ambayo bila shaka anaowakusudia ni wale watu wa kambi ya upinzani (UKAWA) vile vile TAHADHARI hiyo inamuhusu kila Mtanzania anaependelea mageuzi …..ni wajibu wetu kuifanyia kazi .

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s