Matokeo Jimbo la Mahonda bado kitendawili

Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda, Balozi Seif Ali Iddi
                                       Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda, Balozi Seif Ali Iddi
Salma Said, Mwananchi
 
Zanzibar: Bado kitendawili hakijateguliwa katika kinyanganyiro cha kura za maoni ambazo zimeanza kupigwa kwa siku ya tatu katika maeneo mbali mbali nchini.

 
Katika maeneo mengine kura hizo tayari zimeshahesabiwa na kutolewa matokea lakini baadhi ya majimbo kura hizo zimelazimika kurejea baada ya kutokea khitilafu katika uchaguzi huo ikiwemo jimbo la Mahonda ambalo linawaniwa na Makamo wa Rais Balozi Seif Ali Iddi kwa nafasi ya uwakilishi na Ubunge Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar, na Mbunge wa zamani Bi Kidawa Hamid Saleh.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mulla Othman Zubeir alisema katika jimbo la Mahonda tayari matawi 11 yameshapigwa kura na matokeo yake kujulikana isipokuwa limebaki tawi moja ambalo ndilo linalosubiriwa.
Mulla amesema katika uchaguzi wa juzi ulilazimika kurejewa kutokana na khitilafu za hapa na pale lakini hadi sasa unaendelea vyema na matokeo yake yatari yameanza kukusanywa ambapo kwa upande wa Uwakilishi wanaoongoza ni Makamo wa Rais Balozi Seif Ali Iddi ambaye anaongoza kwa kura 1638 dhidi ya mpinzani wake Faraji Ramadhani ambaye amepata kura 441 katika matawi hayo 11.
 
Alisema kazi kubwa ipo katika nafasi ya Ubunge ambapo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na mke wa Naibu Katibu Mkuu Vuai Ali Vuai, Bi Kidawa Hamid Saleh anakabiliwa na upinzani mkali dhidi ya mwanamke mwenzake Bi Bahati Ali Abeid.
Hatima ya Bi Kidawa itajulikana baada ya kuhesabiwa kura za tawi moja lililobakia ambalo lina wapiga kura 320, ambapo Bi Bahati anaongoza kwa kura 1081 wakati mpinzani wake Bi Kidawa amepata kura 700.
 
 “Limebaki tawi moja ambalo lina wapiga kura 320 lakini hata wote wamkatae Balozi Seif basi atashinda kutokana na kura alizopata katika matawi hayo 11 ambazo ni kura 1638 na anayesindana naye  Faraji Ramadhan amepata kura 441, na Ubunge Bi Kidawa amepata kura 700 na Bahati kura 1081, tuvuteni subira ili tupate matokeo sahihi” amesema Katibu huyo.
Katika majimbo mengine sura nyingi mpya zimeibuka na zile za zamani zimeachwa na wananchi katika kinyanganyiro hicho ambacho kimekuwa na mchuano mkali.
Katika jimbo la Nungwi Mbunge na Mwakilishi wote ni wapya ambapo Mbunge ni Mustafa Makame Hamad wakati Mwakilishi amepata Ame Haji Ame.
 
Katika jimbo la Tumbatu Haji Omar Kheri ambaye ni waziri wa nchi ofisi ya Rais anayeshughulikia Idara Maalumu ya Vikosi vya SMZ amefanikiwa kushikilia nafasi yake lakini Mbunge wa zamani amaeangushwa na kupata Juma Othman Hija.
 
Jimbo la Mkwajuni mbunge na Mwakilishi wa zamani wote wameangushwa na kupatikana wapya ambapo nafasi ya uwakilishi kwa sasa inashirikiwa na Ussi Yahya Haji na Ubunge Khamis Ali Vuai.
 
Chaani nafasi ya Uwakilishi imekwenda kwa Nadir Abdulatif Jussa wakati nafasi ya Ubunge imechukuliwa na  Khamis Yahya Machano, katika Jimbo la Bumbwini pia zimekuja sura mpya ambazo uwakilishi inashikiliwa na mwanamke Bi Mtumwa Peya Yussuf na Ubunge Mbarouk Juma Khatib.
 
Jimbo la Donge ambalo kwa zaidi ya miaka 20 linashikiliwa na Ali Juma Shamhuna mara hii limechukuliwa na katibu Mkuu wa ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Dk Khalid Salum Mohamed na nafasi ya Ubunge inashikiliwa na Sadifa Juma Khamis.
 
Jimbo jipya la Kiwengwa limekwenda kwa Mwanamke BI Asha Abdallah Mussa na Ubunge umekwenda kwa Makame Mshimba Mabrouk ambaye ametoka kwenye uwakilishi na kukimbilia kwenye ubunge. Jimbo la Kijini bado matokeo yake hayajapatikana.

 

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s