Hamad Rashid awa mwanachama namba moja ADC

Hamad Rashid Mohamed akionyesha vitendea kazi vya Chama cha ADC, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti, Said Miraji Abdullah (kushoto) jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Doyo Hassan Doyo. Picha: Mwananchi
Hamad Rashid Mohamed akionyesha vitendea kazi vya Chama cha ADC, baada ya kukabidhiwa na Mwenyekiti, Said Miraji Abdullah (kushoto) jana jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Doyo Hassan Doyo. Picha: Mwananchi

Dar es Salaam. Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed amejiunga rasmi na Chama cha Alliance for Democtratic Change (ADC) chenye wanachama wanaokaribia 450,000 lakini akakabidhiwa kadi namba moja aliyosema inampa tiketi ya kuwania urais kupitia chama hicho Zanzibar.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi hiyo na kuikabidhi ya CUF kwa Mwenyekiti wa ADC, Said Miraj, Hamad alisema anawania urais kupitia chama hicho na kwamba Julai 26 atachukua fomu.

Alitamba kwamba anao uzoefu katika duru za siasa, kuanzia chama tawala CCM kabla ya kutimuliwa na kujiunga na CUF ambacho nacho kilimtimua.

“Nimefukuzwa mara mbili, na hiyo yote ni kutokana na misimamo yangu… tunakubaliana jambo, kwa nini tupinde? Ninapopinga kupinda ninaonekana msaliti, lakini huwa ninasimamia uamuzi tunaokubaliana,” alisema.

Alisema hana kashfa hali inayompasisha kuwa anaweza kuwania urais huku akiwataka wanachama wenzake kutambue uwepo wa Mungu ili kupambana na rushwa, ufisadi na ubadhirifu… “Huwezi kupambana na rushwa, au kuwa mwadilifu kama huna hofu ya Mungu.”

Alisema kama watu watabadilika, Tanzania inaweza kupiga hatua na kuleta mageuzi hasa katika kilimo.

Aliwataka wanachama wake kutoingiwa na unyonge mbele ya vyama vingine na wajiamini akisema kufanya hivyo kutakipa nguvu na kuwa kati ya vyama makini.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa

Akizungumzia Serikali ya Umoja wa Kitaifa, SUK, alisema:

“Tumejiwekea mkakati kufanya kazi kwa pamoja, kati ya CUF na CCM, lakini viongozi tunashindwa kusimamia misingi na kuacha Serikali ya CCM ikitawala utendaji wa SUK,” alisema.

Alisema wakati umefika wa kuwapo mabadiliko ya fikra ikiwamo kujipanga kwa maendeleo ya uchumi wa viwanda… “Maendeleo si kupata ruzuku, maendeleo si kupigania majimbo au uongozi.

“Tumekubaliana kuwa CUF itasimamia serikali tatu, lakini baadaye wanasema Bara serikali tatu halafu eti Zanzibar serikali ya mkataba, tofauti kabisa na makubaliano yetu.

Aliwaasa viongozi wenzake wa ADC kutokuwa na nongwa na watakaoamua kukihama chama huku akiwataka kuwatafakari wagombea wanaorudiarudia kuwania urais huku wakidunda mara zote lakini wapo na kwamba ni wakati wa wananchi kuamua kwa kuwa vyama havina utaratibu wa kuandaa watu.

Kauli ya Mwenyekiti

Awali, Miraji alimtaka Rais Jakaya Kikwete kukutana na viongozi wa juu wa vyama vya siasa, kuzungumzia mustakabali wa Taifa kabla hajaondoka madarakani.

Alisema pia kuwa ADC haikatai umoja wowote wenye lengo la kuleta mabadiliko katika nchi lakini  kinachokwaza ni watu kugawana vyeo, majimbo, kufikiria ruzuku.

Chanzo: Mwananchi

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s