Hongera vyama Z’bar kusaini maadili ya uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha
     Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha

Hatimaye vyama vya siasa visiwani Zanzibar vimekubali kusaini mkataba wa Maadili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, baada ya mkutano wa awali kuvunjika kwa madai ya kukosekana wadau muhimu kwenye mkutano huo ambao ni Chama cha Mapinduzi (CCM) na Jeshi la Polisi.

Makubaliano ya maadili hayo ya uchaguzi yalitakiwa yasainiwe kwenye kikao hicho baina ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), iliyoongozwa na mwenyekiti wake, Jecha Salum Jecha na viongozi wa vyama vya siasa kw ajili ya kuweka mwongozo kwa vyama vya siasa wakati wote wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Oktoba 25 ili ufanyike kwa uhuru na haki.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kabla ya kuvunjika kwa kikao cha awali, mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe, Ismail Jussa alisema hawatasaini waraka wa maadili hayo, hadi kitakapoingizwa kipengele kitakachoeleza wazi majukumu ya Jeshi la Polisi na vikosi vya Serikali ya Zanzibar ambavyo alidai vimeonyesha ishara mbaya hivi karibuni.

Jussa alisema kifungu cha 15 kwenye wajibu wa Serikali na wajibu wa ZEC kiongezwe wajibu wa Jeshi la Polisi na wajibu wa vikosi vya SMZ, na kwamba wajibu wa Jeshi la Polisi uwe ni kuhakikisha wanalinda usalama wa raia na mali zao, wapigakura na maofisa wa tume, lakini pia kuhakikisha wanalinda amani na usalama na hawaingiliwi na taasisi nyingine ya ulinzi kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka ya ulinzi.

Jussa alisema licha ya kuwa vikosi vya SMZ havitakiwi kisheria kusimamia uchaguzi, vimeshuhudiwa vikiingilia uandikishaji wa wapigakura na kufanya ukiukwaji mkubwa wa haki za binaadamu, kukiuka sheria, kanuni na taratibu za uandikishaji, jambo ambalo alisema limesababisha kuwapo kwa malalamiko mengi ya wananchi na wadau.

Hatuna pingamizi na malalamiko ya wapinzani, lakini pia tunaunga mkono vipengele vya maadili ambavyo miongoni mwake ni kupinga matumizi ya siasa ya aina yoyote ya kutumia viongozi, wanachama, wafuasi kwa malengo ya kufanya hujuma katika harakati za kisiasa.

Aidha maadili hayo yanakataza vikundi vya ulinzi vya vyama kutumiwa kwa malengo ya kuchochea fujo na kuvuruga amani wakati wa kampeni na uchaguzi.

Hakuna ambaye hafahamu kwamba Zanzibar imekuwa kwenye historia ya siasa za uhasama kwa kipindi kirefu, na uhasama huu hujitokeza zaidi wakati wa uchaguzi hasa kwa vyama viwili vya siasa, CCM na CUF.

Mgogoro wa kisiasa Zanzibar haukuishia tu kwenye vyama hivyo, bali ulisambaa hadi ndani ya familia kiasi cha kujengeana chuki, kununiana, kutosaidiana na kunyimana hada huduma zinazostahiki malipo kwa mujibu wa sheria.

Tunapenda kuvipongeza vyama vya siasa Zanzibar na ZEC kwa kufikia mwafaka huo, ambao tunaamini kwamba utakuwa mwarobaini kwa siasa za uhasama ambazo zimewahi kuitia doa Tanzania kwa kuzalisha wakimbizi waliokimbilia eneo la Shimoni, Mombasa nchini Kenya.

Ni imani yetu kwamba mkataba wa maadili ya uchaguzi utaviwezesha vyama vya siasa kufanya shughuli zao za kisiasa kwa njia ya kistaarabu, kutowaingiza wananchi kwenye uchonganishi wa kisiasa na kwamba siasa kwao ziwe ni matukio ya kupita.

Tunaamini mwafaka uliofikiwa hadi kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na kutiwa saini mkataba wa maadili ya uchaguzi, ni msingi imara wa kuelekea katika Zanzibar iliyo bora, imara na yenye mshikamano kwa wananchi wake.

Ni imani yetu kwamba yale yaliyokubaliwa kwenye mkataba wa maadili ya uchaguzi yatatekelezwa na vyama vyote. Ni vizuri kwa Jeshi la Polisi na vikosi vya ulinzi na usalama pia kuheshimu mkataba huo na kufanya kazi ya kuulinda ili kuweka mazingira mazuri kwa uchaguzi ambao utatoa viongozi wa Zanzibar wa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Advertisements

One Reply to “Hongera vyama Z’bar kusaini maadili ya uchaguzi”

  1. Je CCM itawafanya nini viongozi wao wa matusi na maovu kama Borafia, Asha Bakari na Balozi Seif Ali Iddi?

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s