Magufuli apata mapokezi ya kishindo Zanzibar

Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Mgufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakitoka Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwenda Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Mjini Zanzibar kwa ajili ya utambulisho jana. Picha: Mwananchi
Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Mgufuli na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wakiwapungia mikono wananchi walipokuwa wakitoka Uwanja wa Ndege wa Zanzibar kwenda Ofisi Kuu ya CCM, Kisiwandui Mjini Zanzibar kwa ajili ya utambulisho jana. Picha: Mwananchi

Zanzibar. Mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli jana alipata mapokezi ya kishindo alipokwenda Zanzibar kujitambulisha baada ya kuteuliwa na chama hicho wiki iliyopita.

Akizungumza na wafuasi wa chama hicho katika ofisi ya CCM, Kisiwandui, Dk Magufuli alirejea kauli yake kuwa hivi sasa CCM ipo imara na wagombea wote walioshiriki katika mchakato wa kutafuta mgombea wamevunja kambi zao na kutangaza kumuunga mkono.

Dk Magufuli ambaye alifuatana na mgombea wake mwenza, Samia Suluhu Hassan alisema lengo la CCM ni kushinda katika uchaguzi huku kaulimbiu yao ikiwa ni umoja ni ushindi.

“Sisi tulijitokeza wengi katika kinyang’anyiro hiki lakini kwenye wengi wanachaguliwa wachache, mwisho anateuliwa mmoja lakini mimi nimezungumza na wagombea wenzangu ambao wote wamenikubalia kwamba wataniunga mkono katika safari yetu hii na nina imani kubwa ya kushinda urais wa Muungano kwa kuwa umoja ni ushindi,” alisema.

Akitoa ahadi mbele ya wana CCM, Dk Magufuli alisema akichaguliwa kuwa rais atahakikisha kwamba anaulinda Muungano kwa kufanya kazi na mgombea urais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein ambaye alimsifu kwa umakini wake na ujasiri wake katika uongozi.

“Ndugu wanachama wa CCM, mimi nimefanya kazi kwa karibu sana na Dk Shein katika Baraza la Mawaziri, ni kiongozi hodari, shupavu asiye na maringo na tabia yake ya ucheshi kwa kila mtu inawafurahisha wengi,” alisema Dk Magufuli ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi.

Alisema moja ya kazi kubwa atakazozifanya ni kuulinda Muungano kama kitambulisho na kielelezo ya wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar lakini pia atahakikisha Mapinduzi ya Zanzibar yanalindwa na kuheshimiwa.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Zanzibar, Dk Magufuli pamoja na msafara wake walisafiri kwa gari la wazi huku wakishangiliwa na wafuasi wa CCM hadi Kisiwandui.

Katika mkutano huo, Dk Shein alisema utekelezaji wa Ilani ya CCM ndiyo pigo kwa wapinzani.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s