Aliyenusurika shambulio la Polisi alonga

Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi D/IGP, Abrahaman Kaniki  akimjulia hali askari aliyejeruhiwa wakati wa tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi Stakishari Konstebo Gaston Shadrack na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kamanda wa Polisi  Kanda Maalum ya Dar es Salaam,  Suleiman Kova
Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi D/IGP, Abrahaman Kaniki akimjulia hali askari aliyejeruhiwa wakati wa tukio la uvamizi wa kituo cha Polisi Stakishari Konstebo Gaston Shadrack na kulazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova

Dar es Salaam. Siku moja baada ya watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi kuvamia kituo cha Polisi Stakishari kuua na kupora silaha, mmoja wa walionusurika katika tukio hilo askari Gaston Shadrack amesimulia hali ilivyokuwa.

Askari huyo aliyejeruhiwa bega la kulia na kifua kwenye uvamizi huo juzi usiku alisema alikuwa kwenye lindo kituoni hapo kabla ya wanaume wanane kufika na kudai wamedhulumiana.

“Ilikuwa saa 4 kuelekea saa 5 usiku. Lilikuja kundi la wanaume wanane wakiwa wamevaa makoti makubwa lakini hawajafunika nyuso. Walikuwa wakilalamika, “haiwezekani unidhulumu’ huku wakielekea ndani ya kituo.”

Aliongeza kuwa: “Utaratibu wetu ni lazima mtu akifika apite getini kwa mlinzi kwa ajili ya kupewa maelekezo ili aende ndani. Ila wao walitaka kwenda moja kwa moja,” alisimulia Shadrack ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH).

Kutokana na utaratibu huo wa kuanzia getini, aliwaita watu hao kwa ajili ya kupata maelekezo ya kwenda ndani. Wakati huo akiwa na askari wenzake wanne hapo nje.

“…Kitendo cha kuwaita na kuwauliza mnakwenda wapi, wale jamaa waligeuka na kuvua makoti kumbe ndani walikuwa na bunduki. Wakaanza kutushambulia mimi na askari wenzangu ambao walianguka chini huku wengine wakifyatua risasi juu, nikageuka haraka na kulalia tumbo lakini wakati nageuka jambazi mmoja alinipiga risasi ikanipata kwenye bega la kulia na kifuani,” alisema Shadrack huku akionyesha majeraha hayo.

Alisema baada ya hapo majambazi hao waliingia kituoni na kuendelea kufyatua risasi lakini mmoja wao alibaki nje ya kituo.

“Nilitumia mwanya huo kunyanyua bunduki niliyokuwa nayo na kumfyatulia risasi akandondoka na mimi nikakimbia.”

Polisi kuzikwa na mama yake

Katika hatua nyingine, mmoja kati ya askari polisi wanne waliouawa katika tukio hilo, atazikwa siku moja na mama yake ambaye alifariki dunia baada ya kusikia kifo cha mwanaye, Koplo Gaudin.

Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa Polisi Ukonga, Mrakibu Mwandamizi, Jiliyo Simba alisema, mama wa askari huyo, alipoteza maisha baada ya kupokea habari za msiba wa mwanaye.

“Mama wa Koplo Gaudin alikuwa mgonjwa na alipopokea taarifa za kifo cha mwanaye naye alifariki dunia,” alisema.

 Chanzo: Mwananchi

One Reply to “Aliyenusurika shambulio la Polisi alonga”

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s