Ni Shein na Maalim Seif

Dk Ali Mohammed Shein akisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad
Dk Ali Mohammed Shein akisalimiana na Maalim Seif Sharif Hamad

Dodoma. Halmashauri Kuu ya CCM imempitisha Dk Ali Mohamed Shein kupeperusha bendera ya chama hicho katika kinyang’anyiro cha urais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa awamu ya pili.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliwaambia wanahabari jana kuwa halmashauri kuu ya chama hicho iliyokuwa imeketi jioni ilimuidhinisha mwanasiasa huyo kuwania kiti hicho ikiwa ni awamu yake ya mwisho.

Uteuzi huo wa Dk Shein ulikuwa ni moja ya ajenda za kikao cha halmashauri hiyo ambayo pia ilikuwa na kazi nzito ya kuteua wagombea watatu wa urais wa Muungano kati ya watano waliokuwa wamepitishwa na Kamati Kuu kutoka kwenye kundi la makada 38 juzi.

Kuteuliwa kwa Dk Shein kunarudisha upinzani mkali kwa mara nyingine dhidi ya mgombea wa urais kwa tiketi ya CUF, Maalim Seif Shariff Hamad katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.

Wawili hao waligombea mwaka 2010 na kukabana koo katika uchaguzi visiwani humo ambao ulishuhudia Dk Shein akimwacha Seif kwa tofauti ya asilimia moja.

Matokeo hayo yalifuatiwa na kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Shein akiwa Rais na Maalim Seif, Makamu wa Kwanza wa Rais baada ya kufanyika marekebisho ya Katiba mwaka huo.

Dk Shein alichukua fomu mapema wiki tatu zilizopita pasipo kuwa na mpinzani hivyo kumtengenezea njia nyeupe ya kupitishwa na CCM.

Hata hivyo, safari hii mbali na kupitishwa na CCM kuwania urais, Dk Shein atakuwa na kibarua kigumu kulinda SUK kutokana na CUF kumaliza vibaya katika Serikali hiyo baada ya mawaziri kutoka chama hicho kutoka katika Baraza la Wawakilishi na kusababisha bajeti ya SMZ ipite bila upande wa pili.

Pia, msuguano huo uliendelea zaidi pale wabunge wa CCM walipokataa Maalim Seif kutoingia ndani ya Baraza hilo kukaa eneo maalumu wakati Dk Shein anapolivunja mwezi uliopita jambo lililozua hisia tofauti juu ya mustakabali wa SUK.

Akizungumza wakati wa kurudisha fomu ya kugombea urais mwishoni mwa mwezi uliopita, Dk Shein aliwataka wanasiasa visiwani humo kuacha kutumia SUK kama ngao ya kuvuruga amani kinyume na madhumuni ya kuanzishwa kwake mwaka 2010.

Chanzo: Mwananchi

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s